Wakazi awatolea uvivu Wasanii adai hawajitambui, wanataka kuwa kama Diamond

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rapa Wakazi ametoa kauli kali akiwakosoa wasanii kwa kutojitambua na kutojihusisha na masuala muhimu ya kijamii. Katika andiko lake, alisisitiza kuwa wasanii wengi wamepoteza dira yao ya kuwa kioo cha jamii na badala yake wanataka kuwa matajiri wakifuatilia mafanikio ya msanii maarufu Diamond. Wakazi alieleza kuwa wasanii hawapo tayari kushiriki katika mapambano ya kijamii, badala yake wanajipendekeza kwa viongozi ili kupata manufaa binafsi.
Aidha, alieleza kuwa wengi wao hawazingatii hata masuala yanayowahusu moja kwa moja, hawajiungi na vyama vya kulinda maslahi yao, na wana mikataba mibovu inayowakandamiza. Pia, aliwashauri wanaharakati kuunga mkono wasanii wanaopigania haki badala ya kuwasusia wale ambao hawasimami na jamii.
Wakazi alihitimisha kwa kusema kuwa wasanii wana nafasi kubwa katika mapambano ya mabadiliko, lakini itakuwa vigumu kufanikisha hili kama njaa itaendelea kuwa tatizo.
Soma => Nay wa Mitego: Asilimia kubwa ya wasanii ni wa Serikali. Tuache uoga wa kukemea mambo ya kikatili na kutegemea Wasanii kupaza sauti
 

Attachments

  • 5985460445567369954.jpg
    141.5 KB · Views: 10
  • 5985460445567369940.jpg
    61.6 KB · Views: 11
Mimi nilishaacha mambo ya kwenda kwenye Shoo za wasanii wasiojielewa.

Bora hela yangu niifanyie mambo ya maana kuliko kumpa mtu ambaye jamii ikipata shida humuoni.
 
Jamaa leo kavuna kwangu point 3 za ushindi
 
Mimi nilishaacha mambo ya kwenda kwenye Shoo za wasanii wasiojielewa.

Bora hela yangu niifanyie mambo ya maana kuliko kumpa mtu ambaye jamii ikipata shida humuoni.
Umewapunguzia nini na wewe umeongeza nini kwenye maisha yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…