BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Zikiwa zimesalia siku chache kuhitimishwa kwa sensa ya watu na makazi ilioanza Agosti 23, 2022, wakazi wa baadhi ya mitaa iliyopo Kimara na Mbezi katika Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam wamedai kutohesabiwa hadi sasa.
Hali hiyo imewafanya baadhi yao kudai kukata tamaa ya kushiriki katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kukamilishwa Agosti 29, 2022.
Akizungumza, Shania Salum, Mkazi wa Kimara Korogwe amesema amesitisha shughuli zake kwa siku mbili akisubiri kufikiwa na makarani lakini hadi leo bado hajafanikiwa kuhesabiwa.
"Nimeamua kuacha taarifa kwa mpangaji mwenzangu lakini jana nilipomuuliza alisema bado makarani hawajafika kuchukua taarifa zetu," amesema.
Pia, Mariam Shabani, Mkazi wa Kimara Mwisho amesema hadi sasa amekata tamaa ya kushiriki katika sensa.
"Kwa kweli nimekata tamaa ya kushiriki katika sensa kwa kuwa nyumba ninayoishi ipo jirani kabisa na barabara lakini leo ni siku ya nne bado sijafikiwa na makarani kuhesabiwa," amesema.
Kwa upande wake, Juma Abdallah, Mkazi wa Mbezi amesema yeye bado hajahesabiwa lakini hajakata tamaa kwani bado siku tatu zimesalia hivyo anaweza kufikiwa na karani muda wowote na kumuwezesha kupata fursa ya kushiriki katika sensa.
Alipotafutwa Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi katka Wilaya ya Ubungo, Geogle Maiga amewataka wananchi wilaya hiyo kuwa wavumilivu kwani kazi hiyo inaendelea na watafikiwa kuhesabiwa.
"Sensa inafanyika kwa siku saba hivyo wasiwe na hofu makarani watawafikia na kuwahesabu," amesema.
Kuhusu changamoto ya vishikwambi kizima chaji, Maiga amesema wamegundua baadhi ya makarani walikuwa hawavichaji ipasavyo na kupelekea chaji kuisha kwa haraka.
"Baada ya kuligundua hilo na kuwaelimisha makarani namna sahihi ya kuchaji vishkwambi vyao kwa kiasi kikubwa changamoto hiyo imepungua,"amesema.