Wakazi wa Dar; Ni kweli nikimpatia adhabu mtoto wangu akiwa amefanya makosa nitashtakiwa kwa unyanyasaji wa mtoto?

Wakazi wa Dar; Ni kweli nikimpatia adhabu mtoto wangu akiwa amefanya makosa nitashtakiwa kwa unyanyasaji wa mtoto?

Organic Live Food

Senior Member
Joined
Aug 2, 2013
Posts
127
Reaction score
236
Wadau habari ya wakati huu.

Mwaka jana nilikuwa Dar maeneo ya tabata kisukulu. Nilienda kumsalimia mjomba.

Katika moja ya maongezi alinieleza mjukuu wake mmoja ambaye hasikii sana na anatabia mbovu

Nilimuuliza nyie mmetulea sn kwa viboko na adhabu ndogondogo mpaka tumenyooka
Vipi huyu mjukuu anawashinda nini?

Mke wa mjomba aliniambia majirani wakisikia ama kuona unampa adhabu mtoto ni bonge la kesi la unyayasaji wa mtoto.
Nilishangaa sana.
Akaongezea hata mtoto asipoonekana mtaani na watoto wenzie ni kesi kuwa unamfungia ndani unamnyanyapaa.

Sasa kumuacha mtoto azurure mtaani si chanzo cha kuongeza vibaka mtaani??

Naomba niulize wakazi wa Dar na mikoani je hili lipo kweli mtaani.?

Nishindwe kumnyoosha mtoto wangu anapopinda?

Ili nisiende magereza?
 
Labda Dar ya nchi nyingine na sio Tz.

Lakini inafuatana na adhabu kuna adhabu ya kumkanya mtoto asirudie kosa nakuna adhabu ambayo ni ukatili kwa mtoto.
Mfano mtoto wa miaka 5 akikosea fimbo tatu tu zinatosha kabisa kumfanya ajutie kosa lake , lakini mtu unakuta anampiga mtoto utadhani anauwa nyoka hiyo haifai kabisa.
 
Back
Top Bottom