Wakazi wa Goma wafanya usafi mji mzima baada ya mzozo uliotokea

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Baada ya kundi la waasi wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) kuuteka mji wa Goma, na waliokuwa wamekimbia vita kurejea majumbani kwao, leo tarehe 1 Februari 2025, kuanzia saa kumi na mbili mpaka saa tano asubuhi, kushirikiana na viongozi wakuu wa kijeshi kwenye kundi hilo, wamefanya usafi kuhakikisha mji huo unakuwa na mazingira rafiki kwa wakazi.

Mji mzima ulizagaa nguo na vifaa vya wanajeshi wa Serikali na nguo za wazalendo, viatu, risasi ni vinginevyo. Kulikuwa pia na maiti zilizokuwa mitaroni, na zenyewe zilikuwa zikiondolewa.

Msemaji mkuu wa AFC/M23 Corneille Nanga, nae ameshiriki zoezi hilo.

View: https://x.com/i/status/1885753084162277604
 
Baada ya kuwa Goma ipo mikononi mwa kundi la waasi wa serikali ya Congo, leo wameamkia kusafisha mji huo uliokuwa umezagaa nguo za jeshi na vifaa vingine vya kijeshi, vitu vilivyotelekezwa na raia wakati wanakimbia, na vingine wakati mali za watu zinaporwa.

Ni zoezi aliloshiliki msemaji mkuu wa AFC/M23, Corenille NANGAA, na kuhimiza mji huo lazima muonekano wake uwe wa kipekee. Pamoja na hilo, pia kulikuwa na maiti zilizozagaa mitaloni, na zenyewe zilikuwa zikiondolewa.

Magari mengi yaliyoachwa na jeshi la Congo, bado yamepaki yalipoachwa, hayajaondolewa. Raia walioweza kuongea na vyombo vya habari, wamefurahia zoezi hilo ukizingatia mazingira yalikuwa machafu zaidi tofauti na awali.

Wameongeza kuwa mpaka sasa, amani imetawala,hakuna anayepolwa mali zake, wanajeshi wa M23 ni wakalimu kwao, wanasalimiana nao.

Badhi wamesema wanaona hawatendewi haki na kundi hilo la M23; ni baada ya kuzuwiliwa kuamkia baa na virabuni, na kuwataka wafanye kazi mida ya asubuhi, huku likiwa jambo geni kwao ambalo hawakuzoea, na kusema hali ikiendelea hivo,hawaoni M23 wakifanya vyema tofauti na uongozi ulioangushwa.
 
Kivu zinaweza kustawi sana chini ya M23 na wananchi wakaanza kuishi kwa amani. Kila la hkeri. Ila suala la m23 kutaka kwenda Kinshasa halikubaliki.
 
inaonekana una support hawa magaidi huna akili alafu unazani taifa unajiundia tu mwenyewe kwenye nchi ya watu
South Sudan na Eritrea waliweza, kwanini hawa washindwe? Serikali ya Kinshasa haina nia ya kufanya maendeleo Eastern Congo na pia hawana nia ya dhati kuipambania zaidi ya kulialia mataifa mengine yakawaingize askari wao katika risks na expenses(uhai na finances) huku ushindi ukipatikana wafaidika ni wao.
Wapambane wenyewe otherwise wakubali eneo liongozwe na hao waasi hadi waunde taifa lao.
 
Kivu zinaweza kustawi sana chini ya M23 na wananchi wakaanza kuishi kwa amani. Kila la hkeri. Ila suala la m23 kutaka kwenda Kinshasa halikubaliki.
Tatizo la wa Africa wengi ni kama tuna matatizo ya akili:
1. Majuzi hao hao wanaoishangilia M23, ndo walikuwa wazalendo na kushilikiana katika vita vya kuwaangamiza.
2. Hao hao, ndo waliokimbilia Rwanda, huku siku za nyuma ndo walikuwa wameandamana kuomba jeshi lao liwaruhusu wavuke mpaka na kuivamia Rwanda.
3. Leo hii wananchi wanajiona wana amani, lakin serikali lazima ihakikishe hiyo amani inavurugwa.

4. M23 yenyewe ukiachilia mbali backup yake, inatakiwa ikae kwao,ina haki. Serikali ya DRC, inatakiwa imiliki maeneo yake.
5. Kubwa na la mwisho, kitu ambacho hamtaki kukielewa, hivi vita vinamtafuta sana Burundi, na ni kwa haya mambo ya ukabila. South Africa nae alishaingilia. Hivi vita haviwezi,kupigani vita mbali na kwako si rahisi kihivyo.

Kuhitimisha kwangu sasa: Hili jambo umoja wa mataifa ndo ungeweza kuliweka sawa. Bahati mbaya, umoja huo ni wa kihuni huni, umelenga masrahi zaidi ya maisha ya raia. Nchi za SADC zipo zitakazolala upande wa DRC. Ila mfano, Mozambique atamtelekeza Rwanda? Uganda ataitelekeza Rwanda? Nguvu kubwa iliyopo nyuma ya huu mgogoro mnaifikilia? Hivyo basi, mpaka pale tu waAfrica watakaa meza moja na kuacha unafiki, wataweza kuliweka sawa.
 
Wananchi wanafuata mshindi(mwenye nguvu). Wakikushangilia usidhani wanakupenda.

Toka M23 waibuke Burundi hajawahi kuwa major player kwenye sakata lao, iweje leo sakata lao "Limtafute sana yeye?"

DRC imeshindwa kuwaletea amani Wakivu zaidi ya 15ml. Kama utawala wa m23 utaweza kuwaletea amani na ustawi basi unawafaa zaidi. Lakini m23 kwenda Kinshasa ni kusambaza mauaji 2500km.
 
Kama wakienda wataleta maendeleo waache waende sio viongozi wajinga wa Africa kukaa kula Mali za raia tu Kila siku Bora kifo kuliko unyonge
 
Historia inatuambia hawawezi kuleta maendeleo. Wataishia kuua na kusumbua watu njia nzima na kisha kuanza kula nchi kama wenzao waliopo Kinshasa leo. Maana wakitaka kuitawala DRC yote lazima wakubaliane na maslahi ya wakubwa.
 
Historia Gani inakuambia nyie wezi serikalini safari hii mnakipata shenzi kabisa mmezoe kuonea raia bado ccm
 
Wananchi wanafuata mshindi(mwenye nguvu). Wakikushangilia usidhani wanakupenda.

Toka M23 waibuke Burundi hajawahi kuwa major player kwenye sakata lao, iweje leo sakata lao "Limtafute sana yeye?"

DRC imeshindwa kuwaletea amani Wakivu zaidi ya 15ml. Kama utawala wa m23 utaweza kuwaletea amani na ustawi basi unawafaa zaidi. Lakini m23 kwenda Kinshasa ni kusambaza mauaji 2500km.
Hapo labda ijulikane ni nchi mbili,basi.Af, unadhani labda ubavu wa M23 kwenda Kinshasa ni upi? Lakini jua wanaweza. Na si kwa nguvu yao, bali kwa nguvu ya anaekanyagiwa sahani. Wazito wote wapo DRC, na kila mmoja anataka ahakikishe anapata chake.
 
Back
Top Bottom