DOKEZO Wakazi wa kata za majengo na machinjioni waishi kwa mateso

DOKEZO Wakazi wa kata za majengo na machinjioni waishi kwa mateso

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

mboji

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2024
Posts
200
Reaction score
242
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, wakazi wa kata tajwa hapo juu wanaishi kwa mateso makubwa toka mwaka 2023 mpaka leo baada ya kufanyika tathmini ya uwanja wa ndege Kigoma na kutokulipwa stahiki zao.

Hadi sasa, wakazi hao waliitwa katika viwanja vya zahati ya machinjioni mnamo mwaka 2023, mwezi wa tano, na kuambiwa kuna upanuzi wa njia ya kupaa ndege, ambayo inatakiwa kuwa kubwa kwa ajili ya ndege kubwa kutua.

Hivyo, kutakuwa na wahanga watakaopaswa kupisha mradi huo na zoezi hilo ni la haraka ambalo inatakiwa wakazi hao wafanyiwe tathmini haraka wapishe upanuzi huo ili mradi uweze kukamilika.

Lakini kinyume na makubaliano hayo, ambayo aliyaleta muwakilishi kutoka Tanrodi Kigoma kwa kumuwakilisha mkurugenzi wa Tanrodi Mkoa, leo watu nyumba zao zinawadondokea na wanashindwa cha kufanya.

Maana waliishafanyiwa tathmini na hawatakiwi kuongeza kitu chochote kwenye eneo hilo. Ukiongeza, hulipwi ulichokiongeza, ni hasara kwako. Waliishawaita waandishi wa habari, wakatoa habari hiyo lakini haikuleta athari yoyote mpaka sasa.

Walimuita mbunge Ngenda Kilumbe, akaliongea bungeni, lakini ni miezi sita sasa na hawaoni utekelezaji wa malipo yao.

Hivyo, wanamuomba Waziri Mbarawa, yeye ndio mwenye dhamana ya hilo pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kushughulikia malipo yao ili waondokane na adha hiyo.
 
Mambo ya hii nchi yanaendeshwa kihuni sana, ni nani aliyewaambia kuwa hutakiwi kuongeza chochote kwanza?
 
Mambo ya hii nchi yanaendeshwa kihuni sana, ni nani aliyewaambia kuwa hutakiwi kuongeza chochote kwanza?
Wathamini majengo ukiishafanyiwa tathimini ukiongeza kitu wao hawakitambui
 
Sheria ya uthamini inasemaje?
Sijaisoma ila wakazi wa maeneo hayo kwenye mkutano walielezwa kuwa kama tathimini hiyo itapita myezi sita itatakiwa iongezwe asilimia tano ya kilichothaminiwa na ikifika mwaka mmoja tathimini inakufa inatakiwa kuanza upya
 
Basi wambie waendelee na mipango ya maendeleo
 
Basi wambie waendelee na mipango ya maendeleo
Hilo ndio wazo lolikuwa lakini mpaka waisome hiyo sheria maana hayo ni maneno waliambiwa kutoka mdomoni kwa mjumbe alioagizwa kutoka tanrodi maana unaweza kufanya shughuri za maendeleo kesho na keshokutwa unaletewa sheria kumbe haisemi hivyo
 
Back
Top Bottom