A
Anonymous
Guest
Suala hilo limekuwa kero kubwa kwa kuwa tunashindwa kupita vizuri watembea kwa miguu, wanaotumia vyomvo vya usafiri ndio kabisa wanapata wakati mgumu
Diwani na Mbunge wana taarifa lakini hakuna hatua zozote ambazo zimefanywa mpaka sasa.
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ambao wanasimamia wanajua kinachoendelea na tumewapigia simu lakini hakuna wanachofanya.
Njia ya kutokea Barabara Kuu zimezibwa na vifusi, tukiuliza wanadai Greda liko Gongo la Mboto.
TARURA WATOA UFAFANUZI
Baada ya JamiiForums kuwasiliana na Meneja wa TARURA, Sigala ambaye anasimamia mradi huo amesema "Tayari tumeanza kusambaza kifusi na kazi inaendelea hadi muda huu (Asubuhi Juni 11, 2024)."