Mdeke_Pileme
JF-Expert Member
- Aug 24, 2013
- 1,596
- 2,226
Wakazi wa kijiji cha Mbwera kata ya Mbuchi wilayani Kibiti, mkoani Pwani , wamekuwa wakining'iniza simu zao katika paa la kibaraza la moja ya nyumba iliyopo kijijini hapo kupata mawasiliano.
Baadhi ya wakazi wakizungumza na ITV wamesema, licha ya maendeleo ya barabara iliyotengenezwa kwa kiwango cha tifu, kutoka eneo maarufu la Muhoro, lililopo kata ya Chumbi kuja kijijini kwao, bado wanakumbwa na changamoto ya ukosefu wa mawasiliano ya simu.