Wakazi wa Manispaa ya Kinondoni wapewa siku 30 kupaka rangi upya nyumba zao na kufunga taa za nje

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wakazi wa Manispaa ya Kinondoni wamepewa siku 30 kupaka rangi upya nyumba zao na kufunga taa za nje, vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria, amesema Meya wa Manispaa hiyo, Songoro Mnyonge.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Juni 24, 2026, Mnyonge alisema agizo hilo linaungwa mkono na masharti ya Sheria ya Afya ya Umma na ni sehemu ya juhudi za kuboresha muonekano, usalama na viwango vya maisha ndani ya manispaa hiyo.

Alisema wamiliki wa nyumba wanawajibika kisheria kutunza majengo yao, ikiwemo kufanya matengenezo na kuyapaka rangi inapohitajika, akisisitiza kuwa hilo si sera mpya bali ni wajibu uliopo kisheria.

"Tunataka manispaa yetu iwe ya kuvutia na yenye muonekano mzuri. Rangi zinazopendekezwa ni nyeupe na kijivu. Wamiliki wa nyumba watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo watapewa notisi ya kufanya maboresho ndani ya siku 30," alisema.

Mnyonge aliongeza kuwa kila kaya inatakiwa kuwa na taa za nje ya nyumba, huku viongozi wa serikali za mitaa wakipewa jukumu la kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa.

Alionya kuwa Halmashauri ya Manispaa itachukua hatua za kisheria dhidi ya wamiliki wa nyumba watakaoshindwa kutimiza masharti hayo ndani ya muda uliowekwa.
 
Mpumbavu huyo meya
 
Kama nyumba yangu haina umeme itakuaje?
Kuweka kibatari nje shida ni upepo na mafuta ya taa.
Dah hata sijui nifanyeje....
 
Masharti ni mepesi sana, hata isipotolewa notisi ni wajibu kupaka rangi nyumba ipendeze na kuweka taa za nje
 
tuanze na pale kariakoo, mpk leo 2026 kuna majengo mengi machakavu tena ni ya udongo, kwa nje yamesilibwa na saruji (plasta), yanatia aibu kaaaaatikati ya jiji

itumike sheria ya mipango miji kuwalazimisha wajenge majengo yanayokidhi sheria ya mipango miji ktk eneo husika. au wauze
kwa upande wa pili serikali yenyewe nayo inaingia lawamani moja kwa moja. mpk leo hii 2026 barabara zote hapo ktkt ya jiji (kariakoo) ni mbovu, hazifanani na hazi ya eneo husika. naomba niishie hapa
 
Na wao wajenga barabara, wafunge taa za barabarani.
Wasambaze maji ya Bomba ya uhakika.
Wasambaze meme usio katika katika hovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…