Mimi ni Mkazi wa Masasi, nilihamia huku miezi kadha iliyopita, moja ya changamoto ambayo niliikuta huku na wenyeji wanadai imekuwepo kwa muda sasa, ni suala la umeme kukatika mara kwa mara.
Huku Masasi kwa kweli inafikia hatua unakasirika na mwisho unaanza kucheka, kuna wakati umeme unakatika kila baada ya nusu saa, kuna wakati unakatika muda mrefu bila kujali ni mchana au usiku.
Hatuelewi tatizo ni nini, hivi sisi si ndio tuna gesi huku, sasa faida yake ni ipi kama hatupati huduma vizuri, inakuwa ni kama tunaomba msaada.
Kuna hasara nyingi zinazotokana na umeme kukatika mara kwa mara, hali hii ni hatarishi kwa kuwa juzikati kuna nyumba iliungua na ilidaiwa ni shoti iliyotokana na umeme kukatika na kurudi japokuwa hakuna uthibitisho juu ya hilo.
TANESCO Mtwara chukueni hatua, mnatuumiza Wananchi, kwani kero hii ipo sana maeneo mengi ya Masasi.
Majibu ya TANESCO ~ TANESCO yaomba radhi umeme kukatika mara kwa mara Lindi na Mtwara, yasema kuna kazi ya kufunga Mifumo Mipya