kazikubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 597
- 148
Wakazi wa Mbagala Kizuiani wametoa kilio chao kwa viongozi wa Serikali ili waweze kuwasaidia kuwaondolea janga la wadudu waitwao Kunguni. Kilio hicho wamekitoa kupitia Times Radio. Katika mahojiano yao na mwandishi walimueleza janga hilo wanalo kwa takriban mwaka mmoja na zaidi.
Hapo awali walikuwa wakiona aibu kueleza wazi tatizo hili hadharani. Kwa sasa maji yapo shingoni na wanaiomba Serikali iwasaidie. Kutokana na maelezo yao wananchi hao wanaamini kuwa Kunguni hao huenda wapo hapo kwa njia ya giza (ushirikina) wakitoa sababu mbalimbali:-
1. Wanadai wadudu hao ukithubutu kuwatia dawa ndio una wa double bora uwaache wakuchakaze wakiwa wachache.
Hawasikii dawa hata kidogo.
2. Wanadai wadudu hao ukiwaanika juani au kuwaunguza na maji ya moto hapo ndio unawaongezea ukali mara dufu.
Wanabchi hao wamedai kuwa kwa sasa wanalala nje ya nyumba zao kuwakwepa kunguni. Wanasema bora kuumwa na mbu lakini siyo kunguni maana washambulia mwanzo mwisho.
Je, Serikali itakuwa sikivu au itadai kuwa hilo halitekelezeki kama madai ya madaktari na walimu?
Tunaomba wanchi wenye imani na mapenzi kwa watanzania tuwasaidie wananchi hawa ili nao waishi kwa amani ndani ya jiji la Dar es salaam. Walitoa kilio chao kupitia kipindi cha DIDA wa Mchops na leo wameamua kurudia kupitia redio hiyo hiyo kupitia kipindi cha Bwana Mkisi cha saa 10 jioni hadi saa 1 usiku wakihisi labda redio ya Mbunge wao iliishiwa betri au mgao wa umeme uliiathiri.
Tuwasaidie watu hawa la sivyo tutapata kazi ya ziada ya kuwaongezea damu.