Mimi ni Mkazi wa Mbutu Kigamboni kwa namba ya Wanambutu, changamoto ya Mbutu, barabara ya kutoka Dege kwenda Mkwajuni mpaka kwenye machimbo ya vifusi ni hatari:
Kwanza naomba niwafahamishe yafuatayo;
1. Barabara zote za Kigamboni zitakazojengwa material yake nikimaanisha kifusi chake kitatoka Mbutu
2. Baadhi ya material ya ujenzi wa SGR yalitoka hapo.
3. Daraja la Tanzanite na yametoka kwetu.
4. Barabara ya Kimbiji material yametoka kwetu Mbutu.
5. Viwanda vya cement vinachukua materia kwetu.
6. Barabara zote na madaraja yaliyoharibiwa na hizi mvua wanategemea kifusi kutoka Mbutu
Jambo la kushangaza sisi ndio tuna Barabara mbovu kupindukia, tunajiona kama hatuna Mwakilishi wa kutusemea. Tumetelekezwa magari ya kifusi usiku kucha yanaharibu Barabara.
Picha/video:
Maelezo ya Picha/Video: Hii ni barabara ya Mbutu, Block E
Tunaomba ujumbe huu uwafikie wengi hasa mamlaka za juu ili wafanye uamuzi wa kutusaidia.