informer 06
Member
- May 11, 2024
- 66
- 49
Kwa ufupi ni kuwa kuna maji taka ambayo yanatoka kwenye majengo ya mtu huyo na kutiririka mitaani siku zote, ikifika muda wa mvua ndio kabisa hali inakuwa mbaya kwa wahusika hao kutiririsha au kufungulia maji machafu ili yaungane na yale ya mvua na kuingia mtaani.
Wananchi tumesharipoti mara kibao kwa Serikali za Mtaa lakini hatuoni jitihada za wahusika kuleta suluhu badala yake tunaendelea kuteseka bila msaada wowote, tukienda kuripoti katika ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wanaishia kusema “Hayo ni mambo ya Serikali za Mtaa karipotini huko”.
Viongozi wa Serikali za Mtaa wenyewe tukiripoti kwao wakienda hapo kwenye hiyo nyumba ambapo maji machafu yanatoka, wanatoka wakitabasamu na hakuna kinachoendelea.
Katika hali ya kusikitisha zipo chemba ambazo zipo karibia na makazi zinafanya harufu kuwa kali kutokana na kutiririsha maji machafu ambayo kuna muda yanakuwa na funza, yanaingia mitaani, inauma sana.
Changamoto hiyo imedumu kwa muda mrefu lakini hatuoni mabadiliko badala yake hali inazidi kuwa mbaya zaidi na inaongeza wasiwasi wa kupata magonjwa.
Kwakuwa yapo majukwaa huru kama JF tunaomba mamlaka za juu kufuatilia suala hili kwa kina ili ambapo kuna uzembe wahusika wawajibike iwe ni kuanzia Serikali za Mtaa pamoja na baadhi ya maafisa wa NEMC ambao tumeripoti kwao na hawajachukua hatua mpaka sasa.