BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Sisi wakazi wa Kijiji cha Kemakorere, Kata ya Nyarero Wilayani Tarime tuna changamoto ya kukosekana kwa huduma ya maji kwa muda wa zaidi ya miezi miwili sasa.
Wanaohusika wangeweza kusingizia kuwa hakuna umeme, lakini umeme upo, mabomba yapo na miundombinu yote ipo lakini maju hakuna na hakuna kiongozi wala ngazi ya Mamlaka inayotoa taarifa kuhusu kinachoendelea.
Tunaomba ujumbe huu ufike Serikalini na wajue kuwa RUWASA wametelekeza ofisi na Wananchi hatuna huduma yam aji, tunalazimika kwenda kuchota kwenye visima ambavyo vingine maji yake sio salama kwa afya.
Soma Pia:
~ Huduma ya maji yarejea Kijiji cha Kemakorere, andiko la Mwanachama wa JF lawafikia RUWASA
~ DAWASA, watu wa Mbezi Luis Makabe mpaka kwa Robert hatuna maji yapata wiki sasa. Mhandisi hapokei simu, namba ya huduma kwa wateja haipatikani