Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Jamani tunaomba kupaza sauti zetu, kwa siku ya jana Mei 15, 2024 ilikuwa siku ngumu zaidi kwa wakazi wanaozunguka eneo la godauni la kuhifadhia 'sodium' kwenye eneo la barabara Mchicha Jijini Dar es Salaam ambapo kulitokea moto ambao haijaelezwa wazi ulitokana na nini.
Barabara za maeneo ya karibu zilifungwa kwa muda wa zaidi ya Saa tano huku Wafanyakazi na wakazi wa maeneo husika tukiathirika kwa kiwango kikubwa na hali hiyo ambapo ilikuwa ikitokea hewa mbaya inayotokana na kuungua kwa malighafi hizo zinazodaiwa kuwa na sumu ambazo sana sana usafirishwa kwenda migodini kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Sisi wakazi wa eneo la karibu hususani familia za Wafanyakazi wa TAZARA tumeathirika kwa kiwango kikubwa, hatujui ni matatizo gani yatakuja kututokea maana harufu ni mbaya japo baada ya kugundua hali hii watu walijitahidi kuvaa barakoa kwa sababu tunasikia zile ni sumu na zinaweza kupelekea madhara endapo Mtu amevuta hewa yake.
Lakini kwa upande wa wafanyakazi kuna taarifa tumepewa kuwa hewa iliyotokana na malighafi hizo kuungua imepelekea madhara ikiwemo baadhi ya watu kuanguka kwa kukosa kupumua vizuri, kukohoa japo suala hilo limezimwa kimyakimya.
Wafanyakazi wengi kwenye eneo hilo wamekuwa wakilalamikia mazingira ya kazi kutozingatia usalama hali ambayo inawaweka kwenye changamoto inayoweza kupelekea kupata magonjwa mbalimbali.
Baada ya tatizo hilo kutokea watu ambao wamekuwa wakipita karibu na eneo hilo walizuiliwa bila kuelezwa changamoto iliyopo.
Zimamoto walifika pale na magari yao kama matano tena makubwa lakini hali ilikuwa mbaya zaidi na walitumia muda mrefu mpaka kufanikiwa kuzima moto huo ambao umesababisha moshi mwingi.
Nitoe wito kwa Serikali kufuatilia suala hili kujua lilikuwaje na namna lilivyopelekea athari kwa wananchi na wafanyakazi wa kiwanda hicho ili ikibainika kuna uzembe wahusika wawajibike.
Pia, niombe Serikali kama inataka kulinda afya kwa Wananchi wake viwanda vyenye malighafi za aina hiyo vipelekwe maeneo ya pembezoni ambao hayapo karibu na makazi ya watu ili kuepusha athari zaidi maana viwanda au godauni za aina hii kuendelea kuwa katikati Mji inapotokea janga madhara yake moja kwa moja yanaenda kuathiri Wananchi.
Pia soma - NEMC yakagua Godauni lililodaiwa kuungua na moshi unaodaiwa kuwa na sumu kuathiri Wananchi