Wananchi wa Kijiji cha Msolokelo, Kata ya Pemba wilayani Mvomero, wameondokana na changamoto ya huduma za mawasiliano baada ya kukamilika kwa mnara wa mtandao.
Kijiji hicho chenye wakazi zaidi ya elfu nne kilikuwa hakina uwezo wa kupiga wala kupokea simu kutokana na ukosefu wa mtandao. Sasa, kupitia mnara huo mpya, wakazi wa Msolokelo wameunganishwa na dunia kupitia simu za mkononi, hatua itakayorahisisha mawasiliano na shughuli zao za kijamii na kiuchumi.