MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 350
- 576
Baadhi ya wanawake ambao waume zao walikuwa wanajeshi wa FRDC(jeshi la DRC), wanahangaika sana baada ya waume zao kufia vitani, wengine wapo kambini ilipo MONUSCO, wengine wamekimbilia nchi jirani ya Rwanda.
Wanawake hao walibaki na watoto. Wanachokiongelea ni kwamba wamefukuzwa kambini walikokuwa wakiishi, na kwamba mpaka sasa wapo wapo tu.
Kwa sasa, walikuwa wamepata hifadhi katika shule mbali mbali, lakini uongozi wa M23, ulitangaza kuwa shule zifunguliwe, na wao wanasema ingelikuwa kambi bado zipo wangeenda kambini.
Uongozi wa kundi la M23 haujatangaza chochote kuhusu hawa watu.