real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,299
Ongezeko hilo la watu kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara linaweza kwa namna moja kuwa ni sehemu ya mikakati ya utawala wa Rais Trump kukabiliana na wahamiaji wasioidhinishwa.
Nairobi, Kenya. Wakenya zaidi ya 100 walifukuzwa nchini Marekani mwaka 2017 idadi ambayo ni kubwa katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Rais Donald Trump.
Kuongezeka kwa idadi ya Wakenya kufukuzwa Marekani kutoka 63 mwaka 2016 hadi 103 mwaka jana inaonyesha ongezeko kubwa la Waafrika kurejeshwa makwao.
Mamlaka za Marekani zimewarejesha jumla ya watu 2,134 kutoka nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara katika mwaka uliopita wa fedha uliomalizika Septemba 30,2017.
Hiyo ilikuwa zaidi ya mara mbili ya watu 920 walioondolewa kutoka Marekani katika kipindi kama hicho mwaka 2016.
Ongezeko hilo la watu kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara linaweza kwa namna moja kuwa ni sehemu ya mikakati ya utawala wa Rais Trump kukabiliana na wahamiaji wasioidhinishwa. Inaweza pia kuhusishwa na tabia yake ya kuzidharau nchi za Kiafrika kama gazeti la New York linalopatikana kwenye mtandao wa New Quartz hivi karibuni lilivyopendekeza katika habari yake juu ya kufukuzwa kwa Waafrika.
Somalia, moja ya nchi nane zilizotajwa katika orodha iliyowekewa msisitizo na Trump juu ya wahamiaji waliopigwa marufuku, ilichangia ongezeko kubwa la Waafrika walioondolewa.
Wasomali 521 waliondolewa mwaka jana ikilinganishwa na 198 waliofukuzwa mwaka 2016. Jumla ya wahamiaji haramu 226,119 walifukuzwa Marekani mwaka 2017 ikilinganishwa na 240,225 mwaka 2016.
Chanzo: Mwananchi