Wakenya 8M. Pekee ndio wenye bima ya Afya, Watanzani ni 18M wanalipia bima ya Afya

Wakenya 8M. Pekee ndio wenye bima ya Afya, Watanzani ni 18M wanalipia bima ya Afya

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Ni asilimia 23 pekee ya watu binafsi waliokuwa wakichangia hazina ya kitaifa ya matibabu-NHIF ambao bado wanachangia bima hiyo tangu kuzuka kwa janga la virusi vya corona.

Afisa mkuu mtendaji wa hazina hiyo Peter Kamunyo aliambia meza yetu ya habari kuwa asilimia 77 ya watu binafsi waliokuwa wakichangia bima hiyo shilingi 500 kila mwezi wamesitisha mchango wao.

Wengi wanaochangia hazina hiyo ni wale waliyojiajiri na wenye biashara ndogo ndogo ambazo huenda ziliporomoka kutokana na athari za janga la corona na kufungwa kwa shughuli za kawaida nchini na kimataifa.

“Hii ni kufikia mwisho wa mwezi Juni. Malipo ya hazina kutoka kwa watu walioajiriwa pia yameshuka kwa kiasi fulani,” alisema.

Hazina hiyo ina wanachama milioni 8.5 lakini kwa sasa ni milioni tano pekee wanaolipa.

Watu wengi katika mpango wa watu binafsi kujilipia walikuwa tayari wameanza kuacha kulipa hata kabla ya janga la virusi vya corona, ni asilimia 35 pekee waliokuwa wakilipa vyema.

Alisema mpango huo hauwezi kujisimamia kwa sababu NHIF hugharamia mara tatu zaidi malipo ya matibabu ya wakenya chini ya mpango huo.

Kamunyo alikuwa akizungumza ofisini mwake baada ya kutia saini makubaliano na kaunti ya Kisumu kulipia wenyeji bima ya matibabu.

Kaunti hiyo itatoa shilingi milioni 22.5 kulipia bima za matibabu familia 45,000 kuambatana na makubaliano yao.

“Hawa ni watu ambao hawawezi kumudu kulipia bima za matibabu. Tuliona tuwasaidiye kupata huduma za matibabu,” naibu gavana wa Kisumu Mathews Owili alisema.

“Kila familia ina takriban watu wanne, kwa hivyo idadi hii ni kama watu laki mbili”.

Malipo ya watu binafsi kwa NHIF yapungua kwa 77%


MY TAKE: Athari za kudorora kwa uchumi Kenya, wananchi wengi wameshindwa kuendelea kulipia bima ya Afya 77% ya hao 8M wameacha kulipia, ni 23% ndio wanalipia hadi sass.
 
Katika nchi ya maziwa na asali, idadi ya wanainchi wenye kulipia Bima ya Afya inaongezeka kwa kasi sana sana
 
Back
Top Bottom