joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Ni wazi kwamba wagombea wakuu wa kiti cha urais Kenya katika uchaguzi wa 2022 wameshajulikana, 1)Raila, 2)Rutto.
Hawa wote sio wageni katika siasa za Kenya, wakenya wanawajua vizuri sana kwasababu walishashika nafasi nyingi tena nafasi za juu sana katika serikali ya Kenya kwa muda mrefu sana, kwahiyo uwezo wao unajulikana ndani na nje ya Kenya.
Ni wazi kwamba nchi ya Kenya ni miongoni mwa nchi ambazo mwelekeo wake wa kisiasa, kijamii na kiuchumi haupo vizuri kabisa, rushwa, malumbano ya kikabila na ukanda, mzigo wa madeni, upungufu wa ajira na gharama za maisha vimekua ni matatizo yanayozidi kuwaumiza wakenya siku hadi siku.
Raila na Rutto wamekua ni sehemu ya viongozi walioifikisha Kenya hapa ilipo, katika vipindi vyao vyote vya uongozi, Hakuna hata mmoja anayeweza kujipiga kifua hadharani na kusema kwamba japo amechangia katika kupunguza kero moja wapo kati ya hizo nilizozitaja, kwa ufupi hakuna hata mmoja mwenye rekodi ya kutukuka katika uongozi wao, karibu wote wanashindwa na Matiang'i kwa mbali sana.
Magufuli alipokua waziri, aliweka rekodi nzuri kuwashinda mawaziri wote akiwemo waziri mkuu aliyekuwepo na wale wastaafu, japo hakuwa na wafuasi wengi ukilinganisha Lowasa na Membe ambao walikuwa wakitajwa Sana kama wanavyotajwa Raila na Rutto, lakini watanzania tuliamua kumchagua Magufuli kutokana na rekodi yake ya uchapakazi bora.
Swali la kujiuliza, Kenya wanatumia vigezo gani vya kuwashabikia Raila na Rutto na kumuacha Matiang'i?, je wakenya wanategemea kupata mabadiliko chanya endapo Rutto au Raila atakua rais, au ni yale yale ya kuchagua viongozi kwa misingi ya ukabila na mara tu baada ya uchaguzi wakenya wote wanaungana kulalamikia rushwa, ukabila, deni la Taifa, mauaji, ukosefu wa ajira na ugumu wa maisha?
Ukweli lazima tuuseme, kwa sisi ambao tupo nje ya Kenya tupo katika nafasi nzuri zaidi ya kutoa mawazo ambayo hayapendelei mtu au kabila lolote.
Kwa hali ya Kenya ilipofikia, hakutatokea mabadiliko yoyote endapo Raila au Rutto atakua rais. Wakenya ambao hawatumii vigezo vya ukabila, uchama, au maeneo walikotoka wanajua wazi kabisa kwamba ukilinganisha uchapaji kazi wa Raila na Rutto, hawawezi kumkaribia Matiang'i.