Wakenya hawaielewi Katiba yao wenyewe!

Katiba mpya sio suluhu ya kila kitu!
 
unajua nii walijadili bungeni kabla ya muswada kupitishwa?
Muda wote huo walikuwa wapi wasibadili,UK amenusa kushindwa anatafuta mbinu za kumuokoa kwa kuchomeka vipengele ambavyo vitamsaidia kuiba kura
Na Raila akichukua wanaogopa ata over haul mfumo wote wa rushwa na ukabila
 
SULUHISHO: Msianzishe kwa nia ya kuridhisha upinzani au kuxima kelele za wananchi muanzishe kwa nia ya dhati ya kuleta mabadiliko na hapo hutaskia kelele za upinzani kma unavyodai.
Kwahiyo na wakenya hawakuwa na nia ya dhati kabisa
 
Kwa kweli kama katiba inayotakiwa ni hii inayotoa Uhuru wa kupitiliza, mtu anamtukana hadi mkuu wa nchi bora tubaki na katiba yetu, ili tuendelee kuheshimiana,
 
Mods wekeni kitufe cha dislike, posts kama hizi zinanipa kinyaa mno.
 
Kwahiyo na wakenya hawakuwa na nia ya dhati kabisa
Kenya hakuna chama dola kila chama kinajua kitapita tu kwa hiyo walianzisha kwa nia njema kabisa sema mchakato ukaingiliwa na wahuni wachache wenye uroho wa madaraka na ukabila.
tofauti kabisa TZ mambo mengi mnayaanzisha kisiasa tu ila hamnaga nia ya dhati mfano kilimo kwanza,BRN, Mchakato wa katiba , serikali ya umoja wa kitaifa kule zanzibar na mifano mingine kibao huwa HAMTAKI kabisa yawepo sema mnayafanya kwa kuigiza tu ili mjisafishe kwa wananchi na ndio maana yoote yameishia kufeli tu.
 
Katiba mpya sio suluhu ya kila kitu!
Ni suluhu ya mambo mengi maana hutoa muongozo wa mambo yote muhin ya nchi na kila mwananchi anatakiwa kuyafuata so ni kitu muhim sana. Na inaweza kuwa suluhisho la kila kitu kama viongozi hawatoingilia utekelezaji wa katiba hiyo mfano tume huru zanzibar lakini bado mkapa alienda unguja kumshinikiza jecha kufuta matokeo. sasa hapo kuna utekelezaji wa katiba kihaki kabisa???
muhim ni wote kuheshim katiba na inachosema wote tufuate ingawa kwa watu kama magu wanaosema katiba itaishia kabatini tu mpka anyooshe nchi kwanza inatoa picha jinsi katiba zinavyominywa na viongozi na kupelekea KATIBA KUTOKUWA SULUHISHO LA KILA KITU as u said.
 
dont generalise eti BUNGE LIMEPITISHA..... we ulifuatilia step by step na hoja za wapinzani dhidi ya serikali??? Hukuona nguvu kubwa iliyotumiwa na watawala kuhakikisha muswada ule unapitishwa ambao kila mwenye akaili anajua ndio utakuwa kaburi la upinzani mwakani. Ni kama hapa tanzania useme eti RASIMU YA CHENGE ILIRIDHIWA NA BUNGE bila kufuatilia process nzima ndo utagundua wapinzani hoja zao zilitupwa mbali na kwa kutumia mabavu wakaweka mapendekezo ya upande mmoja tu.
Ndio ambacho kinatokea kenya yaani wanataka waweke maamuzi yatakayofavor upande mmoja wakati uchaguzi ni wa watu wote... sasa ulitaka oding afanyeje??
 
acha ubaguzi mkuu... r u sure ODM ipo ujaluoni tu?? hivi hujui ODM ndio chama kikubwa zaidi kenya kwenye uwakilishi bungeni hao jubilee ni ushirikiano tu ila kila chama kikisimama peke ake ODM kipo na wawakilishi wengi zaidi sasa unataka kusema majimbo mengi ya uchaguzi yako ujaluoni???
Acha ubaguzi wa kiccm kule zenji unaosema cuf ni ya machotara na mahizbu afu ccm cha watu weusi.
 
Ya Kenya hayakuhusu ndewe wala sikio.
Kalb wahed!
Sindano imekuingia vilivyo [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] pole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…