Wakenya huwa mnazikana wapi?

Wakenya huwa mnazikana wapi?

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Nina swali dogo kwa watu wanaotoka Kenya hasa Nairobi, au hata wale waliowahi kuishi huko! Nilikuwa Nairobi kwa muda kidogo lakini kilichonishangaza sijawahi kuona Makaburi (cemetery) kama ilivyo hapa kwetu ambapo kila mahali utaona kuna sehemu maalumu iliyotengwa kwa ajili ya kuzikwa wafu, kwa mfano Makaburi ya Kinondoni, Kisutu, Sinza n.k Je, Wakenya huwa mnazikana wapi? Nyumbani au Mashambani? Ningependa tu kujua!
 
ulikua Nairobi wapi? Nairobi si kijiji, no jiji lililopangwa.

Najua, ni mji mzuri na unavutia sana kwa kweli lazima nikiri, nilikuwa South B, Kilimani,nikaenda Lang'ata, nikazunguka Kileleshwa mpaka Westlands na mwishowe Gigiri na Muthaiga!
Ingawaje una wageni wengi (foreigners) sana kiasi kwamba saa nyingine hauwezi kujua uko nchi gani kwa maana kila mtu anaongea Lugha yake na amevaa kivyake, lkn hilo ni swala lingine!

Ila sikuwahi kuona Makaburi, yaani sehemu maalumu iliyotengwa na Serikali kwa ajili ya kuzikwa Wafu katika sehemu zote hizo nilizopita, ndio maana nikajiuliza hilo swali, Je, Kenya (Nairobi) huwa mnazika Uani kwenu au Shambani, kwa maana kwetu mara nyingi huwa tunazika kwenye makaburi yaliyotengwa maalumu na Serikali? Je, na nyie ni hivyo hivyo au vipi?
 
kuna makaburi ya langata,pia wakenye wana tabia ya kusafiriasha miili ya marehemu kwenda kuzikwa vijijini kwao.
maiti inaweza ikahifadhiwa takribani miezi miwili wakiwa bado wanachangisha hela za kusafirisha mwili.
tatu ka nchi ni kadogo na miundo mbinu za barabara ziko poa so sio issue kusafirisha mwilo.
 
Najua, ni mji mzuri na unavutia sana kwa kweli lazima nikiri, nilikuwa South B, Kilimani,nikaenda Lang'ata, nikazunguka Kileleshwa mpaka Westlands na mwishowe Gigiri na Muthaiga!
Ingawaje una wageni wengi (foreigners) sana kiasi kwamba saa nyingine hauwezi kujua uko nchi gani kwa maana kila mtu anaongea Lugha yake na amevaa kivyake, lkn hilo ni swala lingine!

Ila sikuwahi kuona Makaburi, yaani sehemu maalumu iliyotengwa na Serikali kwa ajili ya kuzikwa Wafu katika sehemu zote hizo nilizopita, ndio maana nikajiuliza hilo swali, Je, Kenya (Nairobi) huwa mnazika Uani kwenu au Shambani, kwa maana kwetu mara nyingi huwa tunazika kwenye makaburi yaliyotengwa maalumu na Serikali? Je, na nyie ni hivyo hivyo au vipi?

Ulikua Lang'ata na unauliza kama Nairobi ina makaburi? Kamuone daktari wa macho.
 
Nina swali dogo kwa watu wanaotoka Kenya hasa Nairobi, au hata wale waliowahi kuishi huko! Nilikuwa Nairobi kwa muda kidogo lakini kilichonishangaza sijawahi kuona Makaburi (cemetery) kama ilivyo hapa kwetu ambapo kila mahali utaona kuna sehemu maalumu iliyotengwa kwa ajili ya kuzikwa wafu, kwa mfano Makaburi ya Kinondoni, Kisutu, Sinza n.k Je, Wakenya huwa mnazikana wapi? Nyumbani au Mashambani? Ningependa tu kujua!

Welcome to Kibera
 
Labda watu wa huko huwa hawafikwi na mauti! Nadhani ni sehemu nzuri ya kuishi!
 
si hutupa maiti zetu kwa indian ocean or maybe lake victoria. kuzikwa ya nini?
 
Back
Top Bottom