ulikua Nairobi wapi? Nairobi si kijiji, no jiji lililopangwa.
Najua, ni mji mzuri na unavutia sana kwa kweli lazima nikiri, nilikuwa South B, Kilimani,nikaenda Lang'ata, nikazunguka Kileleshwa mpaka Westlands na mwishowe Gigiri na Muthaiga!
Ingawaje una wageni wengi (foreigners) sana kiasi kwamba saa nyingine hauwezi kujua uko nchi gani kwa maana kila mtu anaongea Lugha yake na amevaa kivyake, lkn hilo ni swala lingine!
Ila sikuwahi kuona Makaburi, yaani sehemu maalumu iliyotengwa na Serikali kwa ajili ya kuzikwa Wafu katika sehemu zote hizo nilizopita, ndio maana nikajiuliza hilo swali, Je, Kenya (Nairobi) huwa mnazika Uani kwenu au Shambani, kwa maana kwetu mara nyingi huwa tunazika kwenye makaburi yaliyotengwa maalumu na Serikali? Je, na nyie ni hivyo hivyo au vipi?
Nina swali dogo kwa watu wanaotoka Kenya hasa Nairobi, au hata wale waliowahi kuishi huko! Nilikuwa Nairobi kwa muda kidogo lakini kilichonishangaza sijawahi kuona Makaburi (cemetery) kama ilivyo hapa kwetu ambapo kila mahali utaona kuna sehemu maalumu iliyotengwa kwa ajili ya kuzikwa wafu, kwa mfano Makaburi ya Kinondoni, Kisutu, Sinza n.k Je, Wakenya huwa mnazikana wapi? Nyumbani au Mashambani? Ningependa tu kujua!
Hahahaha!!!...I had to laugh at this one...ok go easy on the guy mazee!Ulikua Lang'ata na unauliza kama Nairobi ina makaburi? Kamuone daktari wa macho.
Ulikua Lang'ata na unauliza kama Nairobi ina makaburi? Kamuone daktari wa macho.
Ulikua Lang'ata na unauliza kama Nairobi ina makaburi? Kamuone daktari wa macho.