Wakenya : Mlituwekea kauzibe, Leo Mmesahau?

Kwanza sio kweli kwamba hatujui kinachotokea Ethiopia kwasababu hakuna Uhuru wa habari, hiyo ni sababu mbayotumia kuhalalisha udhahifu wenu, kama mauaji ya watu wa kabila la Oromo yanayofanywa na POLISI wa Ethiopia yanaripotiwa na vyombo mbalimbali na dunia inajua, vipi kuhusu mashambulizi ya Alshabab yatokee Ethiopia dunia isijue?.

Kitu usichojua ni kwamba, jeshi la Amison lilipiundwa kwenda Somalia, kila nchi ilipewa Eneo maalumu la kwenda kukomboa. Uganda walipewa kazi ya kuwatoa Alshabab Mogadishu na viunga vyake, ili kulinda Ikulu na kurudisha Serikali ya Somalia, hiyo kazi walikamilisha, Burundi nao walipewa kukomboa hili Eneo karibu na Mogadishu kama uonavyo katika hiyo ramani. Baada ya Uganda na Burundi kukomboa maeneo waliyopangiwa, kazi kubwa ni kuyalinda na kufundisha jeshi la Somalia ili waweze kujilinda, Uganda na Burundi hawana jukumu la kukomboa maeneo mengine ndio sababu husikii wakisogea hata kilometer moja.

Djibouti yenye askari 900 tu, ndio nchi iliyokomboa sehemu kubwa na wanalinda eneo hilo toka 2015(Block 4).

Kenya na Ethiopia, sio miongoni mwa nchi zilizochaguliwa kuunda jeshi la AMISON, Ethiopia imekua ikishambulia Ethiopia Mara kwa Mara tangu kuanguka kwa Said Barre, kwasababu wanashutumu waasi wa Ethiopia kutoka Jimbo la Somaliland kwamba wanaishambulia Ethiopia na kukimbilia ndani ya Ethiopia, Jeshi la Ethiopia linaingia Somalia sio kwa lengo la kuwapiga Alshabab, lengo lao ni kutengeneza "buffer zone" ili wapinzani wa serikali ya Ethiopia toka jimbo la Somali land ambao wengi ni waisilamu wanapata misaada toka Somalia, kwahiyo majeshi ya Ethiopia yakikaa Somalia kwa muda, huwa yanatoka na kurudi Ethiopia, kumbuka hayapo chini ya Amisom kwahiyo hawapati support ya pesa toka UN.

Kenya ninyi mlienda kwa interest zenu, kwa ujumla ninyi haikujulikana kwa uwazi nini hasa malengo yenu, mwanzo mlisema mnataka kuzuia Alshabab wasishambulie Kenya, tulitegemea mtatengeneza "buffer zone", ghafla mkaanza kuzidi kuingia ndani, bila kujiandaa, kwasababu kama lengo lenu lilikua kwenda kukomboa sehemu kubwa ya Somalia, ni wazi kwamba mngejipanga kwenda na jeshi kubwa litakaloweza kuteka sehemu kubwa ya Somalia, matokeo yake mumezidi kusonga mbele mkiwa na askari wachache ukilinganisha na ukubwa wa eneo, sasa mnauliwa kila siku kutokana na poor planning kuanzia mwanzo.

Kwa kifupi, nchi zote zilizochaguliwa kuunda Jeshi la AMISOM, walipewa majukumu na eneo maalumu toka Mwanzo, walijipanga vizuri na walianda vikosi vyao kulingana na ukubwa wa eneo na majukumu waliyopangiwa, ndio sababu hawauliwi sana kama KDF. Ninyi hamkujipanga, mlikurupuka sana, ndio sababu jeshi lenu linapigwa sana na Alshabab kwasababu ya " Poor planning from the beginning due to luck of precise Vision and missions and very poor military intelligence "
 
Huwezi pinga jambo lolote ambalo mwenzako amepost kwa sababu amepost kutoka source, kama una tatizo na hilo report basi ni vyema utafute mwandishi wa hilo ripoti kwa sababu Kafrikan sio mwandishi. Kila mtu mwenye amewahi fuatilia hili jambo bila roho mbaya na Kenya anajua Kenya ilibadilisha mambo Somalia, wewe tu ndio hujui. Kuchukia Kenya ni sawa lakini si sawa kukataa kabisa contributions za Kenya huko Somalia, hata Yesu alisema ya kaisari mpe kaisari. Hamna mtu anayepingana na kilichopostiwa na Kafrican isipokuwa wewe.
 
Kafrikan katumia source ambazo huku tunaita vyanzo uchwara aka vijarida cha hovyo

Kubwa zaidi ni kuwa mpaka sasa KDF yenyewe haijui kama wamepata ushindi Somalia au bado maana hawajui kwa nini wapo Somalia
 
Hahahahaha, hakuna source yoyote ile iliyosema Kenya au nchi moja ndiyo iliyobadilisha hali ya mambo huko Somalia, Actually kuna clip ya video nitakuwekea inamupnyesha kamanda wa jeshi la Uganda Somalia akihojiwa na wana habari akisema Uganda ndio iliyofanya kazi kubwa ya kuwang'oa Alshabab toka Mogadishu ambako waliwanyang'anya silaha nyingi na waliwauwa na kuwadhohofisha sana.

Alicholeta Kafrika ni ramani inayoonyesha maeneo ya Somalia wanayoshikiliwa na majeshi ya nchi Mbalimbali. Hiyo Ramani inaonyesha bado Djibouti pamoja na kuwa na wanajeshi wachache sana(900), ndiyo iliyokomboa sehemu kubwa ya nchi kuliko Kenya yenye wanajeshi 3,400. Kama kigezo ni kukomboa eneo kubwa basi Djibouti ndio ingetajwa kuwa ndio iliyofanya kazi kubwa.
 
Unachojaribu kusema ni kuwa Kenya sasa hivi haiko Amisom?
Tony245, nimeandika kwa kirefu sana na Nina uhakika umeelewa. Kila nchi huko Somalia ilipewa target na malengo na AU kabla ya kwenda Somalia, Kenya na Ethiopia hazikupewa targets wala eneo la kwenda kukomboa huko Somalia, zilijipekeka kwa interest zao. Hivyo kutumia kigezo cha ukubwa wa eneo linaloshikiliwa na nchi huko Somalia kuwa ndio kiashiria cha nchi hiyo ndio iliyofanya kazi kubwa Somalia sio kweli, Uganda na Burundi walipewa jukumu la kukomboa miji mikubwa na eneo dogo kutokana na ugumu wa maeneo yenyewe kuwa ni makazi ya watu sio msitu kama maeneo yaliyopewa Djibouti.

By the way, nchi ikifanya vizuri huwa inatambuliwa rasmi na AU au UN na kukabidhiwa rasmi medali, hili lilifanyika huko DRC baada ya Tanzania kuwashinda M23, mbona halijafanyika kwa KDF huko Somalia, badala yake ninyi mwenyewe ndio mnaamua kujisifia?
 
Kenya has the most powerful military in East Africa, Kenya has the most quality education in East Africa, Kenya is the only Democratic country in East Africa.

When it comes someone is against Kikuyu leaders is murdered. What democracy ur talking about?
 
Wewe jamaa sijui shida yako nini. Wacha yaishe kwani sina time ya kuargue
 
Wewe jamaa sijui shida yako nini. Wacha yaishe kwani sina time ya kuargue
Punguzeni kujisifia, jaribuni kuwa humble kama nchi zingine, hakuna mtu atakayewaandama, "live real humble and Genuine lives"
 
Kama ungekuwa mtu genuine hungepinga facts unazopewa.
Facts ni kusema KDF wamezidi Ethiopia Army huko Somalia wakati Ethiopia Army is 5 times better in all sectors with bigger long experience on field than KDF?. With this type of mentality, expect nothing but hatred from not only Tanzania but other countries as well.
 
Kwani tunacompare ukubwa wa Ethiopia army na KDF ama tunaongea kuhusu contributions za KDF Somalia? Unaona ulivyochanganyikiwa hata hujui tunaongea kuhusu nini?
 
Kwani tunacompare ukubwa wa Ethiopia army na KDF ama tunaongea kuhusu contributions za KDF Somalia? Unaona ulivyochanganyikiwa hata hujui tunaongea kuhusu nini?
Wewe umeona wapi mtu mwenye busara akajisifia kwa kazi nzuri aliyofanya kama sio ulimbukeni, Kumbuka anayejikweza hushushwa". Tulitegemea UN au AU ndio wawasifie na kuwapa nishani iliyotukuka kutokana na kazi nzuri, kamwe hakuna nchi wala organization ya kimataifa wala kutoka Africa iliyotambua utendaji mzuri wa KDF huko Somalia, ninyi wakenya ndio mnaojisifia wenyewe wakati. Mbona Tanzania tulitunukiwa nishani kwa kazi nzuri ya kuwapiga M23, mbona ninyi hamjapewa, nani aliyesema kwamba KDF ndiyo iliyofanya kazi kubwa kuliko nchi zingine zilizoko Somalia?. Punguzeni SIFA za kijinga, " Work in silence and let your success to be your noises ".
 
Umenifanya nizame kwenye research yangu japo sikua nataka lakini sasa imenibidi nikufunze kama mtoto mdogo. Mimi huwa lazy sana lakini usitoroke subiri nakuja na research yangu kuhusu KDF in Somalia.
 
Umenifanya nizame kwenye research yangu japo sikua nataka lakini sasa imenibidi nikufunze kama mtoto mdogo. Mimi huwa lazy sana lakini usitoroke subiri nakuja na research yangu kuhusu KDF in Somalia.
Lazima ionyeshe kwamba Kenya imetambulika kama nchi iliyofanya kazi kubwa kuliko nchi zingine zote. Iwe imetambulika officially.
 
Nasikia kuna wajeda walinajisiwa kabisa.
 
Sasa hilo ni jeshi au maandazi yaani single attack wajeshi zaidi ya 150 wamauawa na wengine wananajisiwa duu....this is Kenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…