Wakenya mnataka nini kwani?

Wakenya mnataka nini kwani?

ushashi

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2016
Posts
375
Reaction score
518
Mlitaka katiba mpya mkatengeneza, mkataka uchaguzi uwe free, fair and transparent na ikawa hivyo na Dunia nzima ikawasifia wakenya Kwa uchaguzi digital, Ruto akashinda, Odinga akaenda mahakamani akapigwa chini Kwa ushahidi wa wazi kutokana na mahakama ilikuwa live on TV's, Serikali ikaingia kazini, kukawa na changamoto ya ukame all over EA, ok tukavuka hapo.

Sasa hivi ni wakati wa mavuno bado mnapiga kelele bei ya UNGA, mnapiga kelele bei ya vitu Iko juu....so how could the price go down if you don't engage in production? Huku kwetu Tanzania saivi bei ya vyakula Iko chini, diesel imeshuka bei ( 2500 /L), tozo zimeondolewa, somehow life is making sense. Nauliza WAKENYA MNATAKA NINI HASA?

Kama ni haki na usawa Hilo msahau kwenye hii Dunia hakuna haki Wala usawa. Labda kama MNATAKA kuuana manake Hilo nalo mnaliweza. Kaeni chini mjiulize MNATAKA NINI HASA.
 
  • Thanks
Reactions: cpt
Hao nyang'au hawajui wanataka nini haswa. Usijisumbue tafadhali, waache kama walivyo🤣🤣
 
Rais mjenga nchi walikua wamepata na ambae angelinda rasilimali lakini sijui kama watafanya lolote kwa vurugu hizo za kila siku na kazi hawafanyi,
 
Kila siku maandamano na sufuria kichwani wakiomba Ruto awape unga wakapige ugali....umesikia wapi Duniani? Hakuna nchi yoyote Duniani serikali inagawa chakula isipokuwa majukumu ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi raia wafanye kazi wapate unga...na sio kuandamana. Huyo Raila Odinga wenu hataweza kuwaletea unga na mkate mezani.Go back to work for your families....mnakera sana mjue
 
Kenya wamegeuka vituko haijawahi kutokea
 
Back
Top Bottom