Tatizo siyo kujua au kutokujua Kiswahili, bali tatizo langu na Wakenya ni kujivunia kutokujua Kiswahili, hapo ndipo ninaposhindwa kuelewa kwani Kiswahili ni Lugha ya Taifa ya Kenya, sasa iweje Mtu ajivunie kutokufahamu Lugha yake ya Taifa?
Tanzania ni aibu kutokujua Kiswahili na wala hakuna anawezea kujivunia hili!
Cha kushangaza zaidi Mkenya huyo huyo anayejivunia hajui Kiswahili, kazi ikitangazwa na UN, Google au au sijui Microsoft kwamba wanahitaji Mtu mwenye uwezo wa kutumia Lugha ya Kiswahili kwa Ufasaha, Wakenya wale wale wasiokitaka Kiswahili na ambao wanajivunia kila siku kutokukifahamu ndiyo wa kwanza kutuma maombi ya kazi na kusema Kiswahili ni lugha yao, na hapo ndipo tatizo langu na Wakenya lilipo!
Ni watu wachache sana wanaojua na kutumia Kiswahili ipasavyo, hata hiyo Tanzania yenu. Au unafikiria ule uharo nyie huandika ndio Kiswahili. Mtu anapokua muwazi na kukuambia hakifahamu Kiswahili vizuri unamchukulia kuwa mjinga, ilhali huo ndio ukweli.
Kiswahili chenyewe bado hakieleweki, maneno mengi yanaendelea kubuniwa kila siku maana hakijaiva. Juzi tu ndio mumejua maana ya 'makinikia', miaka yote wakati mlikua mnaliwa, mlikua mnaita mchanga wa madini.
Nyie majanga kweli, kwanza lugha zenu za asili hamzijui, Kiswahili chenyewe ndio hicho kinazingua, Kingereza lugha ya dunia kimewashinda.
Binafsi nimejikuta kwenye huu upumbavu wa nyie kutuona wajinga kisa tumekiri kutokujua Kiswahili ipasavyo, ipo siku nilitaka tafsiri ya Kiswahili ya maneno kwa mfano kama 'source code', 'software' n.k. Niliishia kuhangaika maana hata wenyewe hamjui.
Sheria zenu zenyewe mumeshindwa kuziandika kwa Kiswahili, na pia hata stakabadhi muhimu. Juzi hapo kuna zabuni imetangazwa ya kiserikali halafu nikakumbana na maneno kama 'Proposal must be written in English'. Wenyewe mnajua mapungufu ya hii lugha lakini kutwa huwa mnajifanya jeuri, hamna kitu cha ovyo kama maskini jeuri asiyetaka ushauri au kuambiwa.
Leo hii nenda hapo kwenye mgahawa Tanzania na uagize 'sharubati' uone jinsi watakushangaa, hadi pale utaagiza 'juisi' ndio utaeleweka.