Wakenya someni hii

Tz boy 4tino

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2014
Posts
1,598
Reaction score
1,822
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametangaza kupiga mnada ng'ombe zaidi ya 10,000 wa nchi za Uganda na Rwanda waliokamatwa katika operesheni inayoendelea nchini.

Mpina alitangaza hayo leo Jumatatu bungeni mjini Dodoma wakati akichangia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2018/2019.

Waziri huyo ambaye alikuwa akijibu hoja zilizoibuliwa na baadhi ya wabunge amesema ng'ombe hao watapigwa mnada wakati wowote kama ilivyofanya kwa ng'ombe 1,325 wa Kenya.

Amesema uhusiano wa Tanzania nchi nyingine washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni mzuri na akisisitiza hakuna ushirikano wa kihalifu.

Mpina amesema walioingiza ng'ombe hao ni wahalifu na wamevunja sheria za nchi na kutahadharisha wafugaji wa nchi jirani kufuata sheria wanapotaka kuingiza mifugo nchini.

My take :

Sasa wale Wakenya wanaohisi Tanzania bado ni shamba la Bibi, walete mifugo yao Tz. Hii serikali ya awamu hii haijaribiwi.

Siku njema Ma Nyangau !
 
ahaaa haaa haaa. serikali hii siyo ya mchezo mchezo.
sheria zifuatwe kwa maslahi mapana ya taifa.
 
Nyie furahieni tu, hamjui ubaya wake, saa hizi mnachukulia kila kitu kisiasa na kimipasho, sawa haina shida.
 
Yakifanywa kwa waganga ni sawa, ila ingekuwa Kenya pasingekalika, ungesikia ujirani mwema, ila wao wenyewe wakipiga risasi ng'ombe 300,000 kwa ajili ya kulinda ardhi ya mabepari sio shida. Ona jinsi wanavyopoteza maisha ya watu bila sababu, mauaji kama haya Kenya ni kama kawaida, wala serikali haishituki
Man kidnapped at gunpoint in Mombasa found dead
 
Kumbe Hapa Kazi Tu ilikuwa ni Opareshen kamata ngombe wakila nyasi? Kweli nyie ni mabongolala kama ingekuwa ni wala albino mnawakamata kwa mtindo huu tungewatambua sana.
 
Kumbe Hapa Kazi Tu ilikuwa ni Opareshen kamata ngombe wakila nyasi? Kweli nyie ni mabongolala kama ingekuwa ni wala albino mnawakamata kwa mtindo huu tungewatambua sana.
No stone will remain unturned under Magufuli, huku kukitokea tatizo linakabiliwa kwa nguvu zote linamalizwa, inabaki historia ya vitabuni tu, albino killings and Kibiti killings, vilitingisha lakini vimekuwa historia, hivi ninyi xtrajudicial killings, insecurity watu kutekwa na kuuliwa hovyo, rushwa na ukabila vimewashinda kabisa hata kuvipunguza kidogo?, hopeless country hiyo.
 
Kumbe Hapa Kazi Tu ilikuwa ni Opareshen kamata ngombe wakila nyasi? Kweli nyie ni mabongolala kama ingekuwa ni wala albino mnawakamata kwa mtindo huu tungewatambua sana.
Ile Uhuru tano tena ni kwa ajili ya kuua mifugo ya wakenya kwenye ardhi ya Kenya, kwa kutumia askari wa kenya wanaolipwa mshahara kutokana na kodi ya wakenya, huku wakitumia siraha zilizonunuliwa kwa kodi ya wakenya. Yote hiyo ni kulinda ardhi ya bepari mzungu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]


Hiyo ndiyo Kenya maajabu ya dunia
 
Ngombe wa Rwanda na Uganda?
Hilo ni changa la macho, tena mchana kweupe

Wanataka kujustfy tukio la Kenya
 
Aisee hongereni kwa kuzidi kulamba dume! Meanwhile hapo darisalama mzee wa vyeti anazidi kupata maziwa[emoji3] [emoji191] [emoji125]
[/IMG]
 
Tulishawastukia wanaogopa hawajui kitakachofata.
Magufuli aliwaambia mchana kweupe kwamba ataendelea kukamata mifugo yote ya Kenya, kama mnaweza jaribuni kukama mifugo ya Tanzania iliyopo Kenya muone litakalowakuta, zaidi ya CS Amina kulalamika na kukimbilia huruma ya ujirani mwema, ninini zaidi machoweza kuifanya Tanzania?, Kenya imefilisika ikiwa na mzigo wa madeni usiolipika

Where Kenya lies in World’s most indebted countries index - Capital Business

Aisee hongereni kwa kuzidi kulamba dume! Meanwhile hapo darisalama mzee wa vyeti anazidi kupata maziwa[emoji3] [emoji191] [emoji125]
[/IMG]View attachment 630684
 
Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati waziri wa mifugo na uvuvi kwa uamuzi wake wa kuchoma vile vifaranga.madhara yanayoweza kutokea kwa kuingiza vifaranga vyenye ugonjwa ni mkubwa sana kuliko kuchoma vifaranga.big up Mh waziri
 
Tumechoka Tanzania kuwa shamba la bibi. Wanaoihurumia Kenya wavuke mpata kwa miguu kwenda Kenya waone kama wataweza kuokota hata kuni kavu wakaachwa salama. Huku kwetu wanachunga wanavyotaka, wachoma mkaa, wanakata miti n.k. INATOSHA!!! Ardhi yetu si No Mans' Land, ni ya Watanzania. Wao yao wamewapa Mabepari, wanakusanya kodi halafu wachungie huku bure!!! No! its enough.
 

Ugandaaa [emoji15][emoji15][emoji15]
Unataka deal la bomba la mafuta life ghafla?

Rwandaaa [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
Tuna anzia wapi?
 
Sidhani kama kuna ukweli,wamemuogopa mkena wakatunga hii ya Uganda na Rwanda ili Ku poza wakenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…