Wakenya waandamana Marekani kupinga serikali

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
7,147
Reaction score
14,699
RAIA wa Kenya wanaoishi nchini Marekani wameandamana wakipinga Serikali yao ya Kenya, ikiwa ni siku 24, kabla ya uchaguzi wa urais wa marudio unaoatarajiwa kufanyika Oktoba 26, mwaka huu.

Raia hao wa Kenya wanaoishi jijini New York wameandamana kwa madai ya kupinga utawala waliouita mbovu unaongozwa na chama tawala, Jubilee chini ya Rais Uhuru Kenyatta.

Maandamano hayo yaliyohusisha maelfu ya raia hao yamefanyika mbele ya makao makuu ya ofisi za Umoja wa Mataifa...

Nina wasiwasi kuna mkono wa Raila kwenye haya maandamano. Wakenya kuweni makini na hawa wanasiasa: Uhuru/Ruto VS Raila, wanataka kuwagawa kwa maslahi yao binafsi badala ya maslahi ya Kenya...
 
Wabebe box bila kulialia bana. Au waje tu waandamane huku huku kama wenzao wasikie utamu wa teargas za Uzbekistan!
 
Wajinga wa mwisho hawa wote.Mbona hawakulalama na kuandamana uongozi mbovu wa Kalonzo na Raila ambayo wamekuwa serikalini miaka 30 lakini hawana matunda yoyote ya kuonyesha ?

Kitui ndiyo hiyo - umaskini ,maji ni shida ,ajira ni shida.
Kibera ya Raila ndio hiyo umaskini umejaa,Nyanza ipo ukimwi hawezi shugulikia ,ufisadi huko hasemi chochote.
 
RAIA wa Kenya wanaoishi nchini Marekani wameandamana wakipinga Serikali yao ya Kenya, ikiwa ni siku 24, kabla ya uchaguzi wa urais wa marudio unaoatarajiwa kufanyika Oktoba 26, mwaka huu.

Raia hao wa Kenya wanaoishi jijini New York wameandamana kwa madai ya kupinga utawala waliouita mbovu unaongozwa na chama tawala, Jubilee chini ya Rais Uhuru Kenyatta.

Maandamano hayo yaliyohusisha maelfu ya raia hao yamefanyika mbele ya makao makuu ya ofisi za Umoja wa Mataifa...

Nina wasiwasi kuna mkono wa Raila kwenye haya maandamano. Wakenya kuweni makini na hawa wanasiasa: Uhuru/Ruto VS Raila, wanataka kuwagawa kwa maslahi yao binafsi badala ya maslahi ya Kenya...
Bishop, sikuelewi vizuri. Unadhani hao wakenya wanaoishi Marekani hawana uwezo wa kujifikiria na kujiamulia wenyewe pasi na kumhusisha binadamu aitwaye Raila? Au labda unadhani hana wafuasi? Waandamanaji walikuwa na nia gani ,je? Hivi una habari ya kuwa chama flani kenya wanataka kupitisha sheria z kuhalalalisha uwizi na kuondoa uwazi na uwabijikaji kwenye uchaguzi?
Nitarudia nilivyo tamka awali: wakenya na wabongo ni tofauti sana katika uelewa wao kwa maswali mengi, siasa ikiwemo.
 
Mbona maandamano jambo la kawaida kwa Wakenya...pande zote jubilee na NASA wanaandamana nyakati tofauti...ndio democracy ya Wakenya...Ukiwaona wanaandamana wao watakuwa na uraia wa Marekani au ni political asylees...ila malalamshi yao yana mwelekeo wa NASA...
 
yaani hawa jamaa wanatisha...hawa...Kuandamana kweli kunahitaji ujasiri...ni hayo tuu...
 
Waje waandamane huku kwao

Waende Somalia, Afghanistan, Venezuela, Saudia au South Sudan kuandamana na siyo nchi tulivu, huru, tajiri, na ya kidemokrasia kama Kenya au waende Rwanda![emoji2]
 
Wajinga wa mwisho hawa wote.Mbona hawakulalama na kuandamana uongozi mbovu wa Kalonzo na Raila ambayo wamekuwa serikalini miaka 30 lakini hawana matunda yoyote ya kuonyesha ?

Kitui ndiyo hiyo - umaskini ,maji ni shida ,ajira ni shida.
Kibera ya Raila ndio hiyo umaskini umejaa,Nyanza ipo ukimwi hawezi shugulikia ,ufisadi huko hasemi chochote.
Aacha upoyoyo, we ujui kuwa rais ndiye kila kitu? hao uliowataja waliwahi kuwa marais ? ni wapi walipewa bajet ya kutosha kutekeleza majukum yao wakashindwa ? na kama walishindwa serikali ilichukua hatua gan ? au we urais unaufananisha mchezaji wa mpira ? kuwa anaweza kununuliwa toka timu flan nakuja kuwa kapten wa hiyo timu,Sasa sijui unataka rais wao atoke wapi ambaye hajawahi kuwa kwenye serikali zilizopita
 
Waende Somalia, Afghanistan, Venezuela, Saudia au South Sudan kuandamana na siyo nchi tulivu, huru, tajiri, na ya kidemokrasia kama Kenya au waende Rwanda![emoji2]
Hizi nchi ulizotaja zipo kundi moja na Kenya according to international security index,
 
Wajinga wa mwisho hawa wote.Mbona hawakulalama na kuandamana uongozi mbovu wa Kalonzo na Raila ambayo wamekuwa serikalini miaka 30 lakini hawana matunda yoyote ya kuonyesha ?

Kitui ndiyo hiyo - umaskini ,maji ni shida ,ajira ni shida.
Kibera ya Raila ndio hiyo umaskini umejaa,Nyanza ipo ukimwi hawezi shugulikia ,ufisadi huko hasemi chochote.

Punguza mihemuko wewe, unafikiri kubadili slum kubwa zaidi Afrika ni kazi ndogo.. South Africa yenye uchumi mara 8 zaidi ya Kenya mpaka leo imeferi kuondoa Slum sembuse Kenya don't make complicated things sound easy
 
Tungeweza kupata majina ya walio andamana, ingeweza kutoa mwanga kidogo.
 
Waende Somalia, Afghanistan, Venezuela, Saudia au South Sudan kuandamana na siyo nchi tulivu, huru, tajiri, na ya kidemokrasia kama Kenya au waende Rwanda![emoji2]
hizo ni nchi za kidikiteita
 
Back
Top Bottom