Wakenya wahoji vigezo vilivyotumika kuisafisha Tanzania kimyakimya

Wakenya wahoji vigezo vilivyotumika kuisafisha Tanzania kimyakimya

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Wakenya wameanza kuhoji serikali yao iwape maelezo ya kina kuhusu vigezo vilivyotumika kuisafisha Tanzania kutoka nchi ambayo siku zote serikali ya Kenya imekua ikisema kwamba imeathiriwa sana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Viongozi wa Kenya wakiongozwa na rais Uhuru Kenyatta wamekua wakiwaeleza na kuwaaminisha wakenya na dunia nzima kwamba watanzania wengi wameambukizwa Corona na Hospital za Tanzania zimejaa wagojwa wa Corona na maiti zimezagaa mitaani.

Kenya ilifunga mipaka yake ya Somalia na Tanzania kwa madai ya kuwakinga wakenya kutokana na maambukizi yanayotokea katika hizo nchi za Somalia na Tanzania.

Wiki chache zilizopita, rais Uhuru Kenyatta wakati akilihutubia taifa la Kenya kuhusu hali ya maambukizi ya Corona, aliwaonya wakenya kuacha kujilinganisha na nchi ambazo zinaficha taarifa za hali ya maambukizi nchini kwao, kwasababu nchi hizo zimeathirika zaidi kuliko Kenya na watu wanakufa kila siku na kuzikwa usiku.

Waziri Macharia na waziri Kagwe kwa wakati tofauti wamesikika wakisisitiza kwamba, watanzania hawatoruhusiwa kuingia Kenya bila kupimwa au kukaa siku 14 za karantini nchini Kenya.

Jambo lililowastua wakenya ni kitendo cha serikali yao kuiweka Tanzania katika orodha ya nchi salaam na kuwaruhusu watanzania kuingia Kenya bila masharti yoyote bila kuwaeleza na kuwatoa hofu walioijenga ndani ya wakenya dhidi ya watanzania.

Soma comments za Wakenya chini ya hii habari.

Kenya reopens its skies to Tanzania in the latest review
 
Bado tunahasira. Hatutaki kusikia chochote! We will reopen for them when we want!!
Tuwasamehe tu. Walikuwa wamejawa hofu ya corona, mabeberu waliwaingiza chaka, corona kwa ngozi hii, haifui dafu
Turudi tufanye biashara
 
Yamebaki na madeni kibao na bado kooona inawagaragaza 😂😂😂😂

Kila siku walikua wanakopa $ 42 million kwa miezi mi4, uliza sasa zilipotowekea? 😂

Halafu ndio wanajiita wenye IQ kubwa na katiba bora Africa 🚮🚮🚮🤒

Huyu Onyango Obbo sasa anajipendekeza kwa Tanzania ama?
 
Wali watuma. Akina eric omondi, king kaka femi 1 na jopo la wasaidiz wao waje wafanye show then wakirejea kenya wawapime covid waka wagundua ni Negative waka amini kumbe kweli lile Taifa lina neema ya Mungu.
 
Wali watuma. Akina eric omondi, king kaka femi 1 na jopo la wasaidiz wao waje wafanye show then wakirejea kenya wawapime covid waka wagundua ni Negative waka amini kumbe kweli lile Taifa lina neema ya Mungu.

Haikuhitaji mbinu ya namna hiyo kujua tz kuko safi,wakora kibao huku wanaendelea na maisha wakiongozwa na barozi wao,ilitosha hao wahojiwe.
 
Tuwasamehe tu. Walikuwa wamejawa hofu ya corona, mabeberu waliwaingiza chaka, corona kwa ngozi hii, haifui dafu
Turudi tufanye biashara
Unajua kwenye hii vita Wakenya wanachezwa shere sn ni kwamba Magu anajua fika kwamba kagusa maslahi binafsi hasa ya viongozi wa Kenya kupitia KQ na ndiyo maana wanaweweseka.
 
Sawa tumewasikia, ila kuruhu ndege zao kuja kwetu lazima takae mezani tuweke mambo sawa, tunahitaji ATCL iwe na route za Kenya tena kwa idadi sawa au zaidi yao.
 
Back
Top Bottom