flyingcrane
JF-Expert Member
- Oct 17, 2014
- 241
- 88
Serikali yetu inataka kupitisha sheria takriban 24 za usalama dhidi ya ugaidi. ikiwa zitapita mambo haya hatatokea:
Tutakosa uhuru wa kuchat fb, twitter na hapa JF kwa kisingizio cha usalama. tutakamatwa na NIS na kupigwa faini ya millioni 5 au kifungo cha miaka mitatu, tusikubali kupimiwa uhuru wetu wa kuwasiliana
NIS itachunguza kukamata washukiwa wa ugaidi na kuwazuia kwa mda wa mwaka mmoja unavyojuwa hawa jamaa walivyokuwa wakatili..
Serikali itanyima vyombo vya habari uwezo wa kutujuza matukio ya kigaidi nchini na udhaifu dhidi ya serikali kama lilivyotokea westigate wanajeshi kuiba
Wakenya tunavyopenda kuandamana serikali inapotukosea na kubeba nguruwe, punda na kumwaga damu chafu mlangoni bungeni kuwaonyesha kutoridhishwa kwetu, haya yote tutanyimwa.
TUTAKUWA KAMA WATUMWA, WANYONGE WASIOKUWA NA HAKI, TUTATESEKA KWA MIAKA MINGI
Serikali itaiba mabilioni bila sisi kuwa na uwezo wa kuikashifu, ukitoa mdomo tu unapotezwa.
Wakenya kenya haiko katika enzi za moi, wala kama utawala wa museveni au mugabe..Kenya ni nchi huru na tupiganie haki zetu kwa lolote lile.
Uhuru ametumia kigezo cha magaidi kupitisha sheria hii ya kidhulma na kikatili. Tunaunga mkono vita dhidi ya Alshabaab, tunaunga mkono pia vipengele vingi katika mabadiliko hayo lakini wakenya tuwe waangalifu sana kupitisha sheria ambazo zitatuumiza kama wananchi
WAKATI WA MAANDAMANO NA KUPINGA SHERIA HIZI NI SASA NA KAMA SI SASA NI SASA HIVI, TUWE TAYARI KUIKOMBOA NCHI KWA LOLOTE LILE