Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakenya walikusanyika kwa wingi na kuanza kuimba kwa nguvu "RUTO MUST GO." Mkutano huo ulilenga kujadili kufukuzwa kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, na umeshuhudia wananchi wakionesha hasira na kutoridhishwa na uongozi wa sasa.
Cheche kali za kisiasa na wakati mwingine vurugu zilishuhudiwa huku Wakenya katika kaunti zote 47 wakitoa maoni kuhusiana na hoja maalum inayolenga kumfurusha Naibu Rais Rigathi Gachagua madarakani.
Katika ukumbi wa Bomas, kaunti ya Nairobi, kikao cha utoaji maoni kilisitishwa baada ya vurugu kuzuka ukumbini.
Hii ni baada ya mwanaharakati Morara Kebaso kubebwa kwa nguvu na kufukuzwa eneo hilo punde alipowasili kutoa maoni yake.
Pia, Soma: Rigathi Gachagua adinda kujiuzulu, asema bila yeye Ruto asingeingia Ikulu
Raia walilalamika vikali, wakidai waandaji walikataza wapinzani wa Gachagua kutoa maoni. Katika kaunti ya Nakuru, kikao cha utoaji maoni kilisitishwa baada ya kudaiwa kuwa hojaji zilikuwa nakala na si halisi. Wafuasi wa Gachagua walidaiwa kuzuiwa kuingia ukumbini, hali iliyosababisha watu kuingia mitaani kulalamikia hali hiyo.
Hoja maalum ya kutaka Gachagua afurushwe iliwasilishwa bungeni na mbunge wa Kibwezi Magharibi, Eckomas Mwengi Mutuse, ikiwa na mashtaka 11, ikiwemo ukabila na ubadhirifu wa mali ya umma. Wakenya wameruhusiwa kutoa maoni kwa mujibu wa kifungu 118 cha katiba.
Jaribio la Naibu Rais kuzuia zoezi la ukusanyaji maoni lilishindikana, na kesi hiyo itatajwa Oktoba 9. Wakati huo, wabunge wamesubiri kusikiliza hoja ya Mutuse na kuamua kama kumtimua au kumweka Gachagua madarakani. Ili hoja ipite, wabunge 233 wanahitajika kuiunga mkono, huku wabunge 291 tayari wamesaini kutaka Gachagua afukuzwe.
Soma:
--> Gachagua akana kudai Ksh.8B ili akubali kuachia nafasi ya Naibu Rais wa Kenya
--> Gachagua awaonya Wabunge: Mmekula hadi mmevimbiwa sasa mnawatapikia Wananchi, kuweni na Heshima basi!