Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Wasafiri waliokamatwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Wasafiri hao wamekamatwa wakati wa msako wa vyeti hivyo uliokuwa ukifanyika katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta katika mji mkuu, Nairobi.
Hii inakuja saa kadhaa baada ya UAE kupiga marufuku utoaji wa vibali vya kusafiria (visa) kwa wasafiri wanaotoka nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na Kenya.
Vyombo vya habari nchini Kenya vinaripoti kuwa marufuku hiyo iliwekwa baada ya wasafiri kutoka Kenya kupatikana na vyeti gushi vya Covid-19 walippowasili katika taifa hilo la Ghuba.
Kenya imekuwa ikirekodi ongezeko la maambukizi ya Covid-19, huku jumla ya watu wenye maambukizi ikifikia 80,102 vikiwemo vifo vya watu 1,427.