Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,176
Wakenya wanafaidika na utawala wa sasa ambapo Wakenya wanapata ajira kwa urahisi Tanzania, pamoja na mambo mengine. Sera za Dr. Slaa zinaashiria kuwa akiingia madarakani, uhondo huo hautakuwepo tena. Wanasahau kuwa KANU pamoja na kuwa chama chenye nguvu sana, kiliondolewa madarakani!Leo nikiwa kwenye daladala, nilikuwa nikisikiliza matangazo ya Amka na BBC. Moja ya habari ya leo ilikuwa kuhusu Uchaguzi wa Tanzania.
Nilishtuka sana kumsikia mwanamke mmoja kutoka Kenya akisema maneno yaliyoko kwenye link hii hapa chini: (jamani jaribuni kuifungua mutamsikia huyo maza alivyokua anaropoka). ni matangazo ya nusu saa lakini utamsikia huyo maza within the first 10 minutes.
Nadhani amesha *i*a na mafisadi tayari.
BBC Swahili - Redio - Amka na BBC
Ukweli unauma...
Wanadhihirisha ujinga wao hadharani. Hali halisi imejionyesha mpaka sasa kuwa mabango, show za wasanii na wingi wa watu waliosombwa kwa malori hauna mvvuto. Watanzania sio wajinga hivyo, wanajua wanachokitaka na watakisema ifikapo Oktoba 31. Wengine humu wanaoishabikia ccm wana woga mkubwa sasa hivi ccm itakapopigwa chini. Katika woga wao huo wanakuwa kama mbuni ambaye anajificha kwa kuingiza kichwa chake kwenye mchanga, anasahau kuwa kichwa chake ni kidogo, lakini mwili wake wote unaonekana.Kwa kweli nilikasirika sana asubuhi, hadi kufikia sehemu nikasema labda BBC wanaipigia debe CCM, kama ukimsikiliza huyo mama anasema amekuwa Tanzania kwa mwezi mmoja tu hivyo hajui lolote kuhusu Tanzania na hawezi kuwaamulia watanzania kwa kusema CCM itashinda si chini ya asimilia 80% hata wale watafiti wa kuchakachua hawakutoa maksi za juu kiasi hicho. Kigezo anachotumia eti ni wingi wa Mabango ya CCM aliyoyaona, Namshauri kama hajui cha kuongea arudi kwao Kenya.
kwa nini ahojiwe mkeii wakati uchaguzi ni wetu wa bongo?
aiseeeiiiiiiii!!!!!!!!!!:A S angry:Ukweli unauma...