Wakenya wanyakua tuzo zote kwenye mbio za Rock City, Tanzania

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Hivi watani zetu kusini mwa nchi yetu mbona kila tukija kwenye mashndano ya mbio lazima tunyakue kila kitu ndani ya nchi yenu, hamna siku itatokea mjitume walau kidogo. Kili marathon huwa tunashinda kila kitu, sasa hii ya Rock City, Mwanza ndio tumefunika kabisa.

Mkiendelea hivi tunakuja kuchukua na madem wenu.....hehehe
Au labda muwe mnaweka mabango ya 'No Kenyans allowed', la sivyo tutawachosha sana..

----------------------------------------------------

Abrahamu Too kutoka Kenya akimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza leo baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:22:45, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo Moris Motima aliyetumia muda wa saa 02:23:19

Abrahamu Too kutoka Kenya ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza leo baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:22:45, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo Moris Motima aliyetumia muda wa saa 02:23:19.

Kivutio katika mbio hizo ilikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza ambae mbali na kuzindua mbio hizo pia alishiriki katika mbio za km 3 akiambatana na viongozi wengine wa serikali.

Nafasi ya tatu katika mbio hizo pia ilichukuliwa Mkenya George Onyacha aliyetumia muda wa saa 02:23:27, ikiwa sekunde chache nyuma ya mpinzani wake.

Katika mbio hizo zilizoanzia na kuhitimishwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo ilishuhudiwa nafasi ya kwanza hadi ya saba zikishikwa na wakimbiaji kutoka nchini Kenya huku nafasi ya nane ikienda kwa Mtanzania Paschal Mombo alietumia muda wa saa 02:30:43.

Akizungumzia siri ya ushindi wake, mbali na kusifia uratibu mzuri wa mbio hizo uliomuwezesha kukimbia bila changamoto yoyote Too alisema ni kujituma kufanya zaidi mazoezi na kukaa kambini muda mrefu ili kufanya vizuri katika michuano ya mwaka huu.

“Maandalizi ya mwaka huu ni mazuri na washiriki wameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka jambo linalotufanya wanariadha kujiwekea mikakati mizuri ili kuweza kukabiliana na ushindani mkali uliopo katika mbio hizi na ninashukuru Mungu nimefanikiwa,” amesema.

Upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni Mkenya Alice Gradys Otero aliyetumia muda wa saa 02:48:18 akifuatiwa na Mkenya mwenzie Tecla Chebet aliyetumia saa 02:54:28 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Mkenya Flavious Kwamboka alietumia muda wa saa 02:57:32.

Mtanzania Brabuelia Bryton kutoka mkoani Moshi alishika nafasi ya sita kwa upande wa wanawake katika mbio hizo akitumia saa 03:14:41.

Washindi wa kwanza katika mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya nane jijini humo waliibuka na kitita cha Sh 4 milioni kila mmoja, washindi wa pili Sh 2 mil na washindi watatu Sh 1,000,000 mil.

Kwa upande wa mbio za km 21 Peter Limo kutoka Kenya aliibuka mshindi wa kwanza baada ya kumaliza kwa muda wa saa 01:05:24, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo George Wayaki aliyetumia muda wa saa 01:05:50.

Nafasi ya tatu katika mbio hizo pia ilichukuliwa Mtanzania Chacha Boy aliyetumia muda wa saa 01:05:59, ikiwa sekunde tisa tu nyuma ya mpinzani wake.

Upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni Mkenya Dorifin Omare aliyetumia muda wa saa 01:17:12 akifuatiwa na Mkenya mwenzie Alice Mogiare aliyetumia saa 01:18:30 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Mkenya Maiselina Issa alietumia muda wa saa 01:19:55.

Mtanzania Siatha Romanus kutoka mkoani Arusha alishika nafasi ya sita kwa upande wa wanawake katika mbio hizo akitumia saa 01:25:58.

Katika mashindano hayo ilishuhudiwa washiriki ambao pia ni wadhamini wa mbio hizo kutoka makampuni ya PUMA, Tiper, NSSF, RedBull, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), New Mwanza Hotel, EF Out door, CF Hospital, KK Security, na kampuni ya uchapishaji ya SDS wakishiriki kikamilifu katika mbio za KM 5 sambamba na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.

Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Naibu Waziri Shonza alisema aliwapongeza washiriki na waandaaji wa mbio hizo na kutoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana kwa pamoja ili kurejesha hadhi ya mchezo wa riadha nchini.

“Tanzania inaweza kurejea katika ramani ya dunia kwenye michezo kama tukijikita katika maandalizi mazuri ya kuibua na kuviendeleza vipaji vya vijana wetu nchini hasa kuanzia ngazi ya shule za msingi,” amesema.

Naye Rais wa Shirikisho la riadha nchini (RT) ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka mbali mbali na kuwapongeza waandaaji wa mbio hizo alisema licha ya wingi wa washiriki kutoka ndani ya nchi bado taifa linakabiliwa na uhaba wa wanaridha wa mbio ndefu yaani km 42 na wachache wanaofanya vizuri kwenye mbio hizo wamekuwa wakishindwa kushiriki mbio kama hizo zinazofanyika ndani ya nchi.

Ni Wakenya Rock City Marathon 2017 | ShaffihDauda
 
Tupmbane na hali zetu serikali kipaumbele chake ni kushuhulikia wezi na mafisadi michezi haina nafasi kwao
 
Watanzania kwa kweli katika tasnia ya michezo hakuna cha kujivunia. hata kwenye riadha kumebakia historia tu kuwa kulikuwa na akina Filbert Bayi.

Tatizo linachangiwa na uhamasishaji. Vyombo vya habari havina hamasa yeyote kwenye michezo zaidi ya kueneza propaganda tu. Hata vyombo vya kitaifa vinaangusha sana sanaa ya michezo. Mfano leo (Jumapili) taarifa ya habari ya saa mbili TBC waliharibu sana kwa namba walivyoripoti habari za rock city marathon. Kwa mtu ambaye hakufuatilia mashindabo haya katika vyombo vingine vya habari angeamini kabisa Watanzania wamefanya vizuri katika mbio hizo.

Kwa aina ile ya kuripoti ni aibu saba kwa chombo kikubwa kama TBC. Walizungusha zungusha habari ili kuficha ukweli. Sijui walishindwa nini kusema wazi kuwa wabongo wamegaragazwa.
 
Kwa kweli Tz huu upande tumechemsha sana, tuna jamii ambayo wapo very talented na hizi mbio, lakini serikali haijaamua. Sad affairs
 
Tuanzie hapa, nani anaweza kutupa historia ya.wenyekitiki wa chama cha riadhaa katika riadhaa?

Nasita kusema kwamba pengine matatizo yanaanzia kwa kuwachagua viongozi wasiokuwa na uzoefu katika michezo hiyo kwa maana ya kushiriki na kupata tuzo kwamba wawaongoze wengine washiriki na kupata tuzo.
 
Shida wasanii wa nchi hii ni kutumika kisiasa badala ya kubaki kwenye profession zao na kuwa neutral. Mkuu MK254, hebu tujuze kama huko kwenu wasanii hununuliwa na vyama vya siasa hususan nyakati za kampeni. Hivi kweli katika mazingira kama haya pamoja na "kujitoa ufahamu" ili kupata vyeo unategemea michezo ipige hatua? Never! Hongereni wakenya. Hata huyo mh anayesemakana kuwa "kivutio" kwa mujibu wa hiyo habari, I am sure, alikuwa kisiasa zaidi kwenye hayo mashindano kuliko kimichezo.
 
Aisee kenya ninawakubali kwenye Athlete,u r smart on this guyz
 
Ethiopia and Kenya produce the best runners cause preys are always fast.
 
Itabidi mtumie mbinu mbadala kama zile wazungu hutumia kuwapa motisha wanariadha Wao wakati wa marathon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…