Wakenya wapania kuwaangusha watanzania kucheza mechi dhidi ya Everton

Majs

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
232
Reaction score
516

Michuano ya SportPesa Super Cup, imeanza kuwa gumzo huku Wakenya wakitamba zaidi kuwa wanataka timu yao ichukue ubingwa na kupata nafasi ya kucheza na Everton ya England.

Bingwa wa michuano hiyo atapata nafasi ya kucheza na Everton kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tayari makundi mawili ya SportPesa Super Cup yametangazwa na yatajumuisha timu za Tanzania Bara, Visiwani na Kenya.

Timu kutoka Tanzania ambao ni wenyeji ni Simba, Yanga, Singida United na Jang'ombe.

Wakati kutoka Kenya ni Gor Mahia, Express na Nakuru All Stars.

Makundi ya michuano hiyo yako hivi; Kundi la kwanza linakwenda kwa mfumo huu, LEopards wanatcheza na Singida na Yanga itawavaa Tusker. Mshindi wa kila upande watakutana kucheza nusu fainali na mshindi atakwenda fainali.

Kundi la pili, Gor Mahia atawavaa Jang'ombe na Simba itakuwa dhidi ya Nakuru. Washindi watakutana kucheza nusu fainali na mshindi atakwenda fainali.

Mashabiki wengi wa soka kutoka Kenya wamekuwa wakiandika mitandaoni kutoa maoni wakizisisitiza hasa Gor Mahia na Leopards kulinda heshima ya Kenya na kupata nafasi hiyo ya kucheza na Everton.

Kwa hisani ya Saleh Jembe
 

oya kwani nyinyi mnachezesha teams zenyu zishindwe au vipi? unategemea teams za Kenya zisafiri hio njia yote na mentality ya kushindwa? Nyie vipi?
 
Waambieni wao bado sana kwa vilabu vya bongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…