Wakenya wapokea mabaki miili ya jamaa zao waliokufa katika jali ya Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines

Wakenya wapokea mabaki miili ya jamaa zao waliokufa katika jali ya Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Wakenya wamekusanyika kupokea mabaki ya miili ya wapendwa wao waliokufa katika ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines

Familia za wahanga wa ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines iliyoanguka mjini Addis Ababa mwezi Machi na kuwauwa watu wote 157 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wamekusanyika mjini Nairobi kwa ajili ya kupokea miili ya jamaa zao.

C61F30BA-516C-4BA7-80D1-7D1161511CE2.jpeg


Wakenya thelathini na wawili walikufa katika ajali hiyo.

Ndege hiyo chapa ET302 kutoka katika mji mkuu wa Ethiopian Addis Ababa kuelekea Nairobi nchini Kenya iliangua muda mfupi baada ya kuondoka.

Vipimo vya vinasaba DNA kuoanisha masalia ya watu 157 waliouawa katika ajali hiyo vilifanyika miezi kadhaa iliyopita baada ya ajali.

90521BD2-653E-42B6-A234-4654E7F924C7.jpeg


Watu kutoka nchi 30 walikuwa wamepanda ndege hiyo huku wengi wao wakiwa ni raia wa Kenya.


Zimekuwa ni siku za huzuni kwa familia za Wakenya 32 waliouawa ambapo watapata fursa kwa mara ya kwanza kutazama masalia ya miili ya wapendwa wao.

Mazishi ya faragha yatafanyika leo Jumatatu , lakini haijawa wazi ikiwa masalia hayo yatatolewa kwa familia zao.

DDF0482B-E449-43FD-9407-6350CBF5C12A.jpeg


Maafisa nchini Ethiopia wanasema miili mingine ambayo bado haijafahamika itazikwa katika kaburi la kumbukumbu litakalowekwa katika eneo la tukio la ajali hiyo.
 
Dah kipindi chote hicho walikuwa hawajazika hayo mabaki?

Poleni kwa mara nyingine.
 
Back
Top Bottom