Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wametoka rai kwa Inspekta Jenerali wa Polisi Japheth Koome kumkamata askari huyu aliyenaswa na kamera mara tu baada ya kumpiga risasi mtu mmoja kwenye maandamano ya Jumatano katika eneo la Mathare, kaunti ya Nairobi.
Baadhi ya watu katika mtandao wa twitter wamesema wanamfahamu kwa Jina 'Moha' na kwamba kawaida hupatikana katika kituo cha Polisi cha Pangani.
Aidha wengine wamesema kuwa wanamfahamu mke wake vilevile mwenye jina Wanjiku ama Wa Marion.
Idara ya Polisi bado haijatoa tamko lolote tangu Jana ambapo picha hizi zilipoanza kuenea mitandaoni.