Wakenya washinikiza kuondolewa kwa masharti ya kuzuia corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191

Baadhi ya makundi ya kijamii nchini Kenya yametishia kufanyamaandamano ya kupinga masharti ya kudhibiti maambukizi ya corona.
Wiki iliyopita Rais Uhuru Kenyatta alipiga marufuku usafiri wa kutoaka na kuingia majimbo matano yanayosadikiwa kuwa na viwango vya juu vya maambukizi ukiwemo mji Mkuu wa Nairobi, kukomesha ongezeko la maabukizi ya ugonjwa wa Covid-19.



Baadhi ya wale ambao walifanya kazi katika hoteli, wanasema wana familia za kulisha lakini waajiri wao wamelazimika kufunga hoteli zaoImage caption: Baadhi ya wale ambao walifanya kazi katika hoteli, wanasema wana familia za kulisha lakini waajiri wao wamelazimika kufunga hoteli zao




Rais Kenyatta pia alipiga marufuku uuzaji wa pombe katika maeneo yaliyowekewa masharti ya usafiri na kuagiza wenye migahawa kuuza vyakula vya kwenda navyo nyumbani.

Bunge la Mwananchi na Muungano wa wananchi wa Citizens Alliance unasema kuwa masharti hayo yanawaathiri wananchi wa kawaida , wakati shughuli za kisiasa zilichangia "kueneza" virusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…