Wakenya watifuana na 'Wazungu' kuhusu umiliki wa Msemo "HAKUNA MATATA"

Wakenya watifuana na 'Wazungu' kuhusu umiliki wa Msemo "HAKUNA MATATA"

AbaMukulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2018
Posts
2,053
Reaction score
3,586
Msemo wa Hakuna Matata ni maarufu sana ukanda huu wa Afrika Mashriki hasa zile sehemu ambazo zinatembelewa sana na watalii.

Msemo huu ulipata umaarufu kwa ngazi za kimataifa kupitia filamu ya Lion King ambapo kulikuwa kuna wimbo maalumu kabisa uitwao hakuna matata.

Kampuni ya kutengeneza filamu iitwayo Walt Disney karibuni imesajili Hatimiliki ya msemo wa HAKUNA MATATA. Kampuni hii imetengeneza filamu ya Iion King.

Hali hii imesababisha mtifuano kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya kuhusu hasa nani anastahiki kupata Hatimiliki kwenye msemo huo.

Historia fupi ya "Hakuna Matata"

Msemo ulipata umaarufu kwenye eneo la Afrika Mashariki baada ya bendi ya Them Mushrooms kutoa kibao matata kilichoenda kwa jina la 'Jambo Bwana'. Hiyo ilikuwa ni mnamo 1982.

Jambo Bwana ya Them Mushrooms

Ndani ya kibao hicho msemo wa Hakuna Matata umetumika sana.

Ndani ya 1983, bendi maarufu ya Bony M ilitengeneza kibao hicho kwa mahadhi ya lugha ya kiingereza lakini sehemu halisi ya kiitikio ilibakizwa kwa lugha ya Kiswahili.

Jambo Bwana ya Bony M

Mwaka 1994, ulitengenezwa wimbo wa HAKUNA MATATA ambao ulitumika kwenye filamu ya Lion king.

Hakuna Matata kwenye Lion King

2018,Walt Disney walijiandikisha kama wamiliki wa msemo huu wakati wakiwa kwenye mchakato wa kuirudia filamu ya Lion King.

Wazungu walituibia rasilimali sasa wameamua kujimilikisha misemo yetu lakini HAKUNA MATATA
 
hakika wakenya wako sahihi hawa Wazungu wanazidi kutuibia kijinga hivi hadi enzi hizi.
Inashangaza msemo ulitumika kwenye wimbo wa 1982 then wao wanakuja kukwapua umiliki 2018.
Huu ni wizi
 
Hahahaha asee

Pia kampuni ya vifaa vya michezo ya Puma pia wametoa kiatu cha mpira kwa jina la HAKUNA MATATA
 
mawakili wa kenya si wanajifanya wanajua sheria sana sasa ni muda wa kufungua madai katika mahakama za kimataifa . Waachane na ile kesi ya ki comedy ya kuwashtaki wayahudi kwa kumuua Yesu.Sasa hii ndio kesi halisi sasa. Watuete na sisi majirani tuwe mashahidi kuwa hakuna matata ni mali yao kabisa na huwa wanatuazima kuutumia huko kwenye mbuga wa wanyama kuwaimbia watalii baada ya kumaliza safari na kupanda mlima kilimanjaro.
 
Wakiitwa mashahidi tuwe mstari wa mbele kwenda kutetea mashemegi zetu. Tusipotee gizani kisa anaeshtakiwa ni muzungu
 
Kwahiyo lugha ya kiswahili imesha chukuliwa hati miliki na mzungu hakuna matata ni lugha ya kiswahili hapo siyo swala la wakenya tu nikama sanaa ya Tingatinga tulivyo ibiwa hati miliki na mjapani kama sikosei
 
Hatimiliki inawahusu waanzilishi wa kitu.
Waanzilishi ni Wakenya.
 
Wakiitwa mashahidi tuwe mstari wa mbele kwenda kutetea mashemegi zetu. Tusipotee gizani kisa anaeshtakiwa ni muzungu
Lakini hapo tumeibiwa waswahili siyo wakenya tu HAKUNA MATATA ni kiswahili mwisho wa siku lugha nzima ya kiswahili itachukuliwa hati miliki na mzungu bepali tutaanza kulipiswa kodi Kwa kuzungumza na kuimbia lugha ya kiswahili
 
Hapana !! sio kila neno la kiswahili ni la waswahili wote. Hii hakuna matata huku bongo sio asili yetu kabisa. Sisi huwa tunasema ' HAKUNA SHIDA, HAKUNA TABU , HAKUNA NOMA' wao ndio neno matata wanalitumia sana. Sisi bongo tumeanza kulitumia kwa kulazimishwa na wazungu wanaokuja kwenye utalii, hujifunza baadhi ya maneno kwao, na kwa kuwa wakenya walitangulia kuanza kuwasiliana nao wanakuwa wameshawafundisha neno hilo. Hivyo utakuta waongoza watalii wengi , wauza vinyago na sanaa za mikono ndio hutumia neno hilo lakini katika matumizi ya kawaida ya mwananchi wa kawaida neno "HAKUNA MATATA " Halipo kabisa
 
hao manyang'au si wanasema wao wanaongea kingereza
wanang'ang'ania kiswahili cha kazi gani

Mungu aliwaumba wakenya akawaambie wakawe wajinga wabishane tu
wakabishe wakawakomeshe watu wengine
dah umefanya nicheke kwa nguvu saana hapa basi nzima nimewaonyesha wapo wanacheka
 
mawakili wa kenya si wanajifanya wanajua sheria sana sasa ni muda wa kufungua madai katika mahakama za kimataifa . Waachane na ile kesi ya ki comedy ya kuwashtaki wayahudi kwa kumuua Yesu.Sasa hii ndio kesi halisi sasa. Watuete na sisi majirani tuwe mashahidi kuwa hakuna matata ni mali yao kabisa na huwa wanatuazima kuutumia huko kwenye mbuga wa wanyama kuwaimbia watalii baada ya kumaliza safari na kupanda mlima kilimanjaro.
why do you think like a goat? you cannot stand another black African on the world stage because of your lack of ambition ?
despicable MOFO
 
why do you think like a goat? you cannot stand another black African on the world stage because of your lack of ambition ?
despicable MOFO
wewe ni mweusi kweli unaendelea kuaabudu hawa manyangau weupe waliowatawala na kuwaibia kila kitu ikiwemo ardhi na sasa wanapora mpaka msemo wenu,mimi naandika kswahili wewe unakuja na uharo wa kizungu hapa!!! kihere here mkubwa wee wa wazungu. Endeleeni kujipendekeza kwao kwa kuwaabudu wao, mila zao na lugha yao mwisho wa siku ndio mtajua maharange sii mboga
 
Back
Top Bottom