Mbao za Mawe
JF-Expert Member
- May 11, 2015
- 23,372
- 54,943
Habarini wanamichezo
Poleni na pilikapilika za hapa na pale hasa hizi tunazokutana nazo kwenye soka letu hapa nchini. Mapungufu ya wazi kwa waamuzi yamegeuka kuwa ni kawaida katika michezo ya ligi.
Utata wa kusimamia na kutafsiri sheria za za soka bado ni kazi ngumu kwao, huwenda tunaweza kusema waamuzi hawa uwezo wao wa kuona kitu na kukitolea maamuzi kwa haraka ni mdogo sana.
Nashukuru kituo cha Azam Tv pia kwa kutusaidia kuonesha madudu yaliyopo kwenye soka la nchi yetu, mara nyingi tunaondoa utata wa maamuzi kwa kutazama picha za marejeo kutoka kwao. Sasa kwa namna ambavyo waamuzi wamekuwa hovyo katika kusimamia sheria 17 za soka je inakuwaje pale wanapochezesha mechi ambazo haziko LIVE.
Kama kwenye nuru utata mkubwa na wa wazi unaonekana tutajuaje yale yanayotokea kwenye mechi ambazo hatuzishuhudii sisi wanamichezo!
TFF waamuzi wenu ni watu wenye mapungufu makubwa kuliko wanadamu wa kawaida, wachache sana wana uwezo mzuri wa kusimamia sheria za soka ila wengi hakuna chochote wanachokijua zaidi ya kuvaa sare mlizowapa na kukimbiakimbia pasipo kujua nini wanafanya pale uwanjani.
Taabu tupu.