Wakili: Deni la Membe kwa Musiba liko palepale

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Posts
16,908
Reaction score
19,123
Dar es Salaam. Wakili Jonathan Mdeme, aliyekuwa akimwakilisha mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Bernard Membe (69) kwenye kesi dhidi ya mwanahabari Cyprian Musiba, amesema deni la waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje kwa Musiba liko palepale na msimamizi wa mirathi ataendelea alipoishia.

Membe ambaye alikuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne, amefariki leo Ijumaa Mei 12, 2023 katika Hospitali ya Kairuki iliyopo Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.

Itakumbukwa kuwa Oktoba 28, 2021, Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam ilimuamuru Musiba anayejitambulisha kama mwanaharakati huru kumlipa Membe fidia ya Sh6 bilioni.

Kitaifa

Wakili: Deni la Membe kwa Musiba liko Dar es Salaam. Wakili Jonathan Mdeme, aliyekuwa akimwakilisha mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Bernard Membe (69) kwenye kesi dhidi ya mwanahabari Cyprian Musiba, amesema deni la waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje kwa Musiba liko palepale na msimamizi wa mirathi ataendelea alipoishia.

Membe ambaye alikuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne, amefariki leo Ijumaa Mei 12, 2023 katika Hospitali ya Kairuki iliyopo Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.
Itakumbukwa kuwa Oktoba 28, 2021, Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam ilimuamuru Musiba anayejitambulisha kama mwanaharakati huru kumlipa Membe fidia ya Sh6 bilioni.

Katika kesi hiyo namba 220 ya mwaka 2018, Membe alimdai Musiba fidia ya Sh10.3 bilioni kwa madai ya kumkashfu kupitia magazeti yake ya Tanzanite.

Akizungumza na Mwananchi leo Mei 12, 2023 kuhusu hatima ya deni hilo, Wakili Mndeme amesema madai dhidi ya Musiba hayatafutika kwa sababu msimamizi wa mirathi ataendelea kufuatilia madeni ya marehemu.

“Katika makosa ya jinai, mtuhumiwa akifariki kesi inaisha hapo, katika makosa ya madai ni tofauti. Anateuliwa msimamizi wa mirathi ya marehemu halafu anavaa viatu vya marehemu kukusanya madeni na mapato kama yapo.

“Kama madeni yanalipwa, kama ni mapato yanagawanywa kwa mrithi halali kwa maana mke na watoto. Kwa hiyo kesi ya madai dhidi ya Musiba ni shauri la madai hivyo halitafutika kwa sababu msimamizi wa mirathi ataendeleza pale alipoishia,” amesema Mndeme.

Amesema kesi iko katika hatua ya kukazia hukumu au utekelezaji wa hukumu na maombi yaliwasilishwa mwaka 2022 na kupewa namba 26 ya mwaka 2022 na Mahakama ya Kuu Dar es Salaam.
Wakili huyo wa Membe amesema alishateuliwa dalali kuendelea na kazi kukazia hukumu.

Kuhusu Membe
Akizungumzia kifo cha mteja wake huyo, Mndeme ameeleza kusikitishwa akisema alikuwa ni mtu mwenye msimamo na kujiamini.

“Mimi sijapoteza tu mteja, bali nimepoteza rafiki yangu na jana nimezungumza naye na kushauariana naye mambo mengi.

“Nimejifunza kufanya kazi na mtu aliyefanya kazi serikalini. Kujiamini na kusimamia msimamo, ukitaka kufanya jambo unalifanya kwa kujiamini na mteja wangu alikuwa anajiamini na kuendesha kesi miaka mitatu katika mazingira magumu,” amesema Wakili Mndeme.

Amesema Membe alikuwa mtu anayepokea ushauri na kwamba hakuwa mbishi na kwamba alikuwa na uwezo na mwenye kumbukumbu sawia na uelewa mkubwa.

Chanzo; Mwanainchi.
https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/membe-afariki-dunia-rais-samia-amlilia-4232080
 
Musiba itabidi arudi tena kwa mganga wake
FB_IMG_1683107648424.jpg
 
Wataalamu wa mambo wana Msemo kwamba: "Actio Personalis Moritur Cum Persona"- a personal action dies with the person" - kwamba matendo ya kibinafsi ya mtu yanakufa na mtu.

Yaani, Mtu akifariki, Madai yake dhidi ya Mtu flani nayo yanakufa, wanaobaki (Wasimamizi wa Mirathi) hawawezi kudai/kudaiwa kile ambacho Marehemu alikuwa anadai/anadaiwa.

Huu Msemo unatumika kwenye baadhi ya kesi kama vile za Kashfa/Kudhalilisha (Defamation), kama ilivyokuwa kesi ya Bernard Membe v. Cyprian Musiba.

Tunajua Mahakama iliamuru Membe alipwe Bilioni 6. Akafungua maombi ya kukazia Hukumu (Application for Execution), pamoja na gharama zingine, nimechungulia mahala anadai si chini ya Bilioni 9.9.

Sasa Membe amefariki akiwa anamdai Musiba hizo Bilioni kadhaa, je amefariki na Madai yake? Musiba Hadaiwi? La hasha! 👇🏿

DENI la Musiba kwa MEMBE liko pale pale. Hii ni kwasababu kesi tayari iliisha na Mahakama ikatoa Hukumu/Amri/Tuzo (DECREE). Amri (DECREE) ya Mahakama ni mali kama mali zingine. Amri ya Mahakama aliyopata Membe dhidi ya Musiba inaingia kwenye Mirathi yake, kwahiyo atakayeteuliwa kuwa Msimamizi wa Mirathi ya Membe ataendelea kumdai Musiba kama kawaida.

Hiyo👆🏿ingekuwa tofauti kama Membe angefariki kabla ya kufungua kesi au kesi ikiwa inaendelea na Hukumu bado haijatoka au Hukumu ingetoka akashindwa halafu akakata rufaa kisha akafariki kabla ya rufaa kuisha, hapa ndipo Membe angefariki na Madai yake na Msemo wa hapo juu ungetumika. Lakini huo Msemo haitumiki kama kesi tayari imeisha , kama ilivyo kesi ya Membe v. Musiba. Hata ingetokea Musiba angekata rufaa kisha Membe afariki kesi ikiwa kwenye rufaa, bado ingeendelea kama kawaida.

Ukipata wasaa, soma maamuzi hayo ya Mahakama ya Juu/Upeo ya India, ambao ni marafiki zetu kwenye sheria, wametafsiri vifungu vya Sheria ya Mirathi ya India (kuna maeneo hata sisi tunaitumia - ona pia PAEA), Sheria ya Mwenendo wa Madai ya India (tumechukua kifungu kama kilivyo - OXXII - CPC) na Sheria ya Mabadiliko ya Sheria - Law Reform Misc. Amendment Act (sisi kwetu ona kifungu 9 Sura 310). Hizi Sheria ndio unaweza kupata Msemo wa Mtu anakufa na matendo yake ya kibinafsi ikiwemo kesi za Kashfa (Defamation), lakini kwa tafsiri ya Mahakama huu Msemo haitumiki kama kesi tayari imeisha na kuna Amri (Decree) ya Mahakama. Kwasababu kesi ya Membe v. Musiba ilishaisha na kuna Amri (Decree) ya Mahakama kumtaka Musiba alipe, Deni lipo palepale hata baada ya kifo cha Membe.✍🏼

MD, Mendez (M.C.A)
14/05/2023
 
Hayatuhusu, kamfufue aje adai hela yake halafu afe tena
 
Itoshe kusema kwamba DENI HALIFI ndio maana unapotokea Msiba watu huulizwa kuna ambae anadaiwa na marehemu au anamdai marehemu ? Km yupo anaemdai wanafamilia uangalia namna ya kumlipa Deni lake na vivyo hivyo' kwa mdaiwa lazima alipe DENI
 
Hilo deni halilipwi , kuanzia mahakama , Yule mfu mpak ww mtoa mada hamna kitu mtafanya , hlo deni likilipwa nakunya mafungu mafungu mpak Chamwino
 
Tumechoka kuzika
 
Sasa Membe amefariki akiwa anamdai Musiba hizo Bilioni kadhaa, je amefariki na Madai yake? Musiba Hadaiwi? La hasha! [emoji1541]

DENI la Musiba kwa MEMBE liko pale pale. Hii ni kwasababu kesi tayari iliisha na Mahakama ikatoa Hukumu/Amri/Tuzo (DECREE). Amri (DECREE) ya Mahakama ni mali kama mali zingine. Amri ya Mahakama aliyopata Membe dhidi ya Musiba inaingia kwenye Mirathi yake, kwahiyo atakayeteuliwa kuwa Msimamizi wa Mirathi ya Membe ataendelea kumdai Musiba kama kawaida.

Hiyo[emoji1540]ingekuwa tofauti kama Membe angefariki kabla ya kufungua kesi au kesi ikiwa inaendelea na Hukumu bado haijatoka au Hukumu ingetoka akashindwa halafu akakata rufaa kisha akafariki kabla ya rufaa kuisha, hapa ndipo Membe angefariki na Madai yake na Msemo wa hapo juu ungetumika. Lakini huo Msemo haitumiki kama kesi tayari imeisha , kama ilivyo kesi ya Membe v. Musiba. Hata ingetokea Musiba angekata rufaa kisha Membe afariki kesi ikiwa kwenye rufaa, bado ingeendelea kama kawaida.

Ukipata wasaa, soma maamuzi hayo ya Mahakama ya Juu/Upeo ya India, ambao ni marafiki zetu kwenye sheria, wametafsiri vifungu vya Sheria ya Mirathi ya India (kuna maeneo hata sisi tunaitumia - ona pia PAEA), Sheria ya Mwenendo wa Madai ya India (tumechukua kifungu kama kilivyo - OXXII - CPC) na Sheria ya Mabadiliko ya Sheria - Law Reform Misc. Amendment Act (sisi kwetu ona kifungu 9 Sura 310). Hizi Sheria ndio unaweza kupata Msemo wa Mtu anakufa na matendo yake ya kibinafsi ikiwemo kesi za Kashfa (Defamation), lakini kwa tafsiri ya Mahakama huu Msemo haitumiki kama kesi tayari imeisha na kuna Amri (Decree) ya Mahakama. Kwasababu kesi ya Membe v. Musiba ilishaisha na kuna Amri (Decree) ya Mahakama kumtaka Musiba alipe, Deni lipo palepale hata baada ya kifo cha Membe.[emoji1600]

MD, Mendez (M.C.A)
14/05/2023
Hivi huwa mnapata wapi muda wa kupoteza kujadili mambo ya wanasiasa ?
 
Itoshe kusema kwamba DENI HALIFI ndio maana unapotokea Msiba watu huulizwa kuna ambae anadaiwa na marehemu au anamdai marehemu ? Km yupo anaemdai wanafamilia uangalia namna ya kumlipa Deni lake na vivyo hivyo' kwa mdaiwa lazima alipe DENI
Ndio iko hivyo
 
Back
Top Bottom