Wakili Harold Sungusia: Kama tunatazama maslahi mapana ya Taifa basi tutatoa mapendekezo ya Katiba Mpya ambayo hayana ubinafsi

Wakili Harold Sungusia: Kama tunatazama maslahi mapana ya Taifa basi tutatoa mapendekezo ya Katiba Mpya ambayo hayana ubinafsi

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807

View: https://www.youtube.com/live/3CV9o7c2fo8?si=_pUk3LIG7gbkpfIq
Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) Wakili Harold Sungusia amewataka washiriki wa Mdahalo wa wazi juu ya mchakato wa kupata katiba Mpya Tanzania kuangalia maslahi mapana ya Taifa na sio maslahi binafsi,au maslahi ya Taasisi,Dini wanazotoka
IMG-20240622-WA0016.jpg

Wakili Sungusia amesema hayo mapema leo Juni 22,2024 jijini Dodoma wakati akitoa neno la ufunguzi kwenye mjadala wa wazi juu ya mchakato wa kupata katiba Mpya Tanzania

"Sisi watanzania hatua tatizo la Afya ya akili kwa hiyo hatuwezi kufanya mambo yale yale huku tukitegemea matokeo tofauti,lazima tutoke hapa tukijiuliza ni jambo gani tufanye tofauti ili tuweze kupata matokeo kwa namna tofauti."

"Lazima tujue jambo gani tunaweza kufanya,ili tuweze kujiindoa kwenye ule mkwamo uliotokea mwaka 2014"amesema

"Kama tunatazama maslahi mapana ya Taifa basi tutatoa mapendekezo ambayo hayana ubinafsi ndani yetu na kwa sababu yatakuwa hayana ubinafsi naamini kutakuwa hakuna mgongano wa maslahi"amesema

Aidha amesema kuwa ubinafsi ndio unaosababisha mgongano wa maslahi.

"Kwa nini Mwalimu Nyerere mwaka 1952 aliandika kitabu chake chenye kurasa 12 tujisahihishe na akasema miongoni mwa matatizo makubwa yanayotukumba Sisi binadamu hasa sisi waafrika ni ubinafsi"amesema
IMG-20240622-WA0018.jpg

Tukiondoa ubinafsi na tukangalia suala la katiba katika jicho Pana la maslahi ya Taifa tutapata zao la katiba ambayo imetokana na amani,tungetamanani kuona tunapata katiba ambayo siyo zao la mgogoro,kwa sababu nchi nyingi zimepata katiba kwa njia ya mgogoro.

Naye Mary Munissi Mwenyekiti wa TLS Mkoa wa Dodoma wakati akitoa neno la Ukaribisho amewapongeza wadau wote walioitikia wito wa mwaliko
Amesema kuwa sote tunajua umuhimu wa kuwa na katiba Mpya na nzuri kwa maendeleo ya nchi yetu.
IMG-20240622-WA0019.jpg

"Tunawashukuru TLS kwa kuandaa mdahalo huu na kuuleta mkoani kwetu Dodoma ili nasi wadau wa Dodoma tupate fursa ya kutoa mchango wetu na tuwe sehemu ya kupata hiyo katiba mpya"amesema

Awali akimkaribisha Rais wa TLS kufungua mjadala huo Mjumbe wa Baraza la Uongozi na Mwenyekiti wa kanda ya kati Laetitia Petro amesema kuwa wananchi wa makundi mbalimbali wameshiriki kikamilifu katika mchakato wa kupata katiba Mpya.
IMG-20240622-WA0020.jpg

"Wananchi hao wote waliweza kupata fursa ya kupitishwa kwenye katiba tuliyonayo kwa kuangazia ubora wake,mapungufu yake na athari Zake za Taifa,pia walipata fursa ya kutoa maoni yao"amesema.
IMG-20240622-WA0021.jpg

Aidha amesema kuwa Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika kinafanya jukumu lake chini ya kifungu cha nne cha Sheria ya Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika Sura ya 307 ya kushauri ,kusaidia Serikali,Bunge,Mahakama na Wananchi kwenye masuala yote ya Sheria
IMG-20240622-WA0022.jpg
 
Back
Top Bottom