Wakili Kambole: Vyombo vya dola vikivunja haki za binadamu wakati wa Maandamano ya amani, hatua za kisheria zitachukiliwa

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058


=======

"Wakati wa Maandamano ya amani, Vyombo vya dola vikivunja haki za binadamu kwa namna yoyote hatua za kisheria zitachukiliwa dhidi yao! Iwapo waandamanaji watafikishwa kwenye vyombo vya sheria msaada wa kisheria upo kwa ajili yao! Ni bora wakalindwa wafanye maandamano kwa amani!"

Wakili Kambole ameendika hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter.
 
Mahakama zipi? Hizi ambazo mnasema haziko huru?
 
Hawa ndo wakati wa Magufuli walikuwa wamesahau kabisa hizo haki za binadaamu ndo zipi..
Walikuwa kiimya kama sio wao..
Kweli Magufuli kafa aisee
 
Afrika bado tunahitaji Maombi ili kuwezesha vijana Wetu Kuwa na uelewa wa kila wanachotamani kukifanya kiwe na maslahi Bora Kwa taifa.

Wawe na uelewa na si mkumbo kwasababu tu wale tunaowaamini wamesema na kutukana.

Polisi hawana haja ya kuzuia maandamano wanatakiwa kuhakikisha yanafanyika Kwa Amani. Mfano huu wa kuruhusu mikuno ya hadhara uenziwe.

Serikali itoe forum ya majadiliano ili ione cha kuchukua na kuacha mwisho wa siku kuwe na maamuzi kulingana na maoni ya wengi.
 
Hawa ndo wakati wa Magufuli walikuwa wamesahau kabisa hizo haki za binadaamu ndo zipi..
Walikuwa kiimya kama sio wao..
Kweli Magufuli kafa aisee
Wakati wa Magufuli kesi zilifunguliwa nyingi mojawapo ni Wakurugenzi kutosimamia uchaguzi na Serikali imeshindwa

Nafikiri kipindi Cha Magufuli ndio alipingwa sana

Huyu Mama hajapingwa hata robo ya Magufuli kama moto wa kumpinga ukiendelea hivi , Mama atatema bungo
 
TOKA MAKTABA :

Tanzania Mission to the United Nations
Geneva, Switzerland

Tanzania yahudhuria Mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu​


Picha : waziri wa sheria na katiba Mh. George Simbachawene akiwa Geneva alipokwenda kuelezea hali ya kisiasa na haki za binadamu iliyopo Tanzania ktk awamu ya 6 . Kumbukumbu: 30 Mar 2022



1. Tanzania yahudhuria Mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu, ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanyiwa tathmini ya Haki za Binadamu. 2. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (Mb.) ameongoza Ujumbe wa Tanzania ambapo ameeleza hatua mbalimbali zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye masuala mbalimbali ya Haki za Binadamu nchini Tanzania ikiwemo Elimu, Afya, Haki za Watoto, Wanawake, wenye ulemavu, Haki za Kisiasa na mengine mengi. 3. Tathmini ya Tanzania imekubaliwa na Baraza hilo, nchi 23 zilizoizungumzia Tanzania kwa hatua nzuri zilizofanyika katika kuhakikisha Haki za Binadamu zinazingatiwa. Pia wamekumbusha Tanzania kuendelea kutatua changamoto zilizobaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…