Wakili Kisabo: Jeshi la Polisi ni miezi mitano halijatekeleza maagizo ya Mahakama kueleza alipo Soka na wenzake

Wakili Kisabo: Jeshi la Polisi ni miezi mitano halijatekeleza maagizo ya Mahakama kueleza alipo Soka na wenzake

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Wakili Paul Kisabo ameeleza kuwa amemuandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) kutaka majibu ya utekelezaji wa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu upelelezi wa walipo Deus Soka, Jacob Mlay, Frank Mbise.


View: https://youtu.be/vEgMlh8IoFI?si=ytSt2Uo8IZ_rnAVx

Wakili huyo ambaye alifungua Kesi ambayo ilitolewa uamuzi na Mahakama ameeleza "Februari 07, 2025 nilimuandikia barua IGP wa Tanzania kutaka majibu ya utekelezaji wa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu upelelezi wa walipo Deus Soka , Jacob Mlay, Frank Mbise. Barua hiyo ameipokea Feb 10, 2025."

"Ikumbukwe kwamba Agosti 22, 2024 nikiwa wakili wa Soka, nilifungua shauri la jinai namba 23998 kudai Deus Soka , Jacob Mlay, Frank Mbise waachiliwe huru baada ya kutekwa. Agosti 28, 2024 Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam iliwaagiza Jeshi la Polisi kufanya upelelezi wa kuwatafuta walipo hawa ndugu zetu, sasa ni zaidi ya miezi 5 hakuna taarifa rasmi kuhusu utekelezaji wa hukumu hiyo."

Amesisitiza kwamba "Maamuzi ya Mahakama Kuu ni lazima yatekelezwe na yanapaswa kutekelezwa kikamilifu. Kwa mujibu wa Sheria za Tanzania ni kosa kutokutekeleza maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania." amesema Wakili Paul Kisabo
 
kumuandikia barua IGP inaweza isijibiwe vilevile
 
20241121_163920.jpg
 
Hao wako chimbo sasa chimbo gani?
Waliyowakamata itakuwa wanaona noma kuwatoa chimbo
Maana wamewashilkilia muda mrefu bila kuwapeleka mahakamani

Nawaza tu hivyo


Ova
 
Kesi ya afande wa dodomya ilifikia wapi?Gari iliyosababisha ajari ya pikipiki ya ndugu yetu wasinza pale external vipi tulishaipata au nimesahau.
 
Back
Top Bottom