Kenya 2022 Wakili: Kura 4,463 zilipunguzwa kutoka kwa Raila na kupewa Ruto

Kenya 2022 Wakili: Kura 4,463 zilipunguzwa kutoka kwa Raila na kupewa Ruto

Kenya 2022 General Election

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Julie Soweto, wakili katika timu ya wanasheria wa kiongozi wa Azimio Raila Odinga, amedai kuwa kura 4,463 zilitolewa kutoka kwa mteja wake na kuongezwa kwa Rais mteule William Ruto katika Kaunti za Bomet, Kiambu, Kakamega, Nairobi na Baringo.

Akizungumza katika mahakama ya Juu siku ya Jumatano bi Soweto pia alilalamika kwamba kulikuwa na tofauti katika fomu 41 za 34A kutoka Bomet, Kiambu na Kakamega zilizopewa maajenti na zile zilizopo kwenye tovuti ya IEBC, ambazo ziliwasilishwa katika kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura cha Bomas.

"IEBC ilinunua seti mbili za fomu 34A licha ya kutakiwa kununua kijitabu kimoja pekee ambacho kingetumiwa katika vituo vya kupigia kura huku 2/2 kikihifadhiwa kwenye bahasha isiyoweza kuguswa. Hati ya kiapo ya Celestine Anyango inaonyesha ubaya wa kimakusudi katika matumizi ya fomu. Fomu ambazo mawakala wanazo na fomu kwenye tovuti ni sawa katika vipengele vyote (namba za mfululizo, mihuri, sahihi). Hata hivyo, takwimu katika fomu zimebadilishwa na ni tofauti," alisema.

Awali, wakili Mkuu James Orengo, ambaye pia katika timu ya wanasheria wa Bw Odinga, alidai kuwa IEBC haina utendakazi na haiwezi kufanya uchaguzi. Pia alidai kuwa fomu hizo zilibadilishwa.
 
Odinga kashindwa kihalali kabisa. Hapo wanapoteza muda tu
 
Tume ilihusika kwenye uchafuzi
 
F61E05AF-05A0-4ABF-833C-7FF720564C72.jpeg
 
Huyo dada kaongea ugoro tu.

Kesi watu wanashinda kwa kutoa ushahidi na sio maneno matupu.
 
Back
Top Bottom