Wakili Peter Madeleka amecharuka katika kesi inayomhusisha Afande Fatma Kigondo, anayekabiliwa na tuhuma za kuratibu tukio la ubakaji wa kundi na ulawiti wa binti wa Yombo Dovya, Dar es Salaam. Madeleka ametaka mshtakiwa akamatwe mara moja kwa kukaidi kufika mahakamani.
Kesi hiyo, ambayo ilipangwa kusikilizwa Oktoba 7, 2024, iliahirishwa hadi leo, Oktoba 15, baada ya Afande Fatma kushindwa kufika kwa madai ya kuwa mgonjwa. Wakili Madeleka amesisitiza kuwa mshtakiwa apewe adhabu kali kwa kukaidi, akisema, "Hatuwezi kuruhusu mahakama ichezewe."
Kwenye ushahidi uliowatia hatiani watuhumiwa victim mwenyewe yule binti alikana kuwa afande aliokua ameambiwa amuombe msamaha alikua anaonyeshwa picha yake kwenye simu na siyo huyo mama, kwahiyo madeleka ajiandae kulipa fidia kwa kumchafua huyo mama

Madeleka kafanikiwa kupata umaarufu ila shida ni kuwa huwa hashindi kesi mahakamani kwasababu ni mtu wa kukurupuka, juzi kati katoka kuharibu kesi ya Eric Kabendera aliyokua anawadai Vodacom fidia ya mabillion baada ya taarifa zake kuvujishwa , Kabendera alichokosea ni kumtumia Madeleka kama wakili wake hatimae alienda kuharibu kesi hoja zake zikatupiliwa mbali alishindwa kudraft vizuri ushahidi wake.