Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Huu ni mkataba, akija mtu akasema kuwa haya ni makubaliano mkatalieni ni muongo. Muongo ni muongo tu. Bunge lilipitisha Mkataba. Bunge halina mamlaka ya kupokea na kujadili na kuridhia makubaliano. Kilichojadiliwa ndani ya bunge la Tanzania ni mkataba.
Vipngozi wa Serikali wanaona labda kwa kuita mkataba huu makubaliano labda kutakuwa na unafuu fulani utakaozima au kuleta unafuu kuhusu mjadala unaoendelea kuhusu ubovu wa huu mkataba kuhusu Serikali ya Tanzania na Dubai.
Baada ya Bunge kuridhia jambo, kinachofuata ni utungaji wa sheria, Dkt. Slaa amekaa bungeni zaidi ya miaka 15 na anafahamu kuwa unapojadili na kuridhia mkataba wa kimataifa, taathira yake ni kufanya huo mkataba kuwa sheria.
Ndio maana kwa kutambua hilo sasa Bunge la JMT limepokea Muswada wa Mabadiliko mbalimbali ya Sheria namba 2 ya mwaka 2023 kwa ajili ya kufanya marekebisho ya sheria zilizopo ili sheria hizo ziweze kuendana na huu mkataba tulioingia kwa sababu utekelezaji wa huu mkataba unahitaji nguvu ya sheria
Pia soma > Serikali imependekeza Sheria zinazolinda Maliasili na Kuikinga Nchi na Mikataba Mibovu zisitumike kwa DP World