Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Jopo la Mawakili wanaomwakilisha Dkt.Wilbrod Slaa kwenye Kesi ya Jinai Namba 993 ya Mwaka 2025 wamewasilisha maombi mawili kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo ombi la kwanza ambalo limesikilizwa leo Januari 23, 2025 walikuwa wanapinga kunyimwa dhamana kwa mteja wao.
Katika ombi la pili ambalo litasikilizwa Januari 24, 2025 kwenye Mahakama hiyo wanapinga uhalali wa kesi ya msingi ambayo ipo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Jopo likiongozwa na Wakili Peter Madeleka pamoja na Wakili Hekima Mwasipu wamewasilisha hoja zao kupinga kunyimwa dhamana kwa mteja wao ambaye alifikishwa kwenye Mahakama ya Kisutu kwa mara ya kwanza January 10, 2025.
Jopo hilo limeeleza Mahakama Kuu kwamba ni haki ya mshtakiwa kupewa dhamana, ambapo wameiomba Mahakama Kuu kufanya mapitio ya kilichofanyika Mahakamani Januari 10,13 na 17, 2025 kwenye kesi ya msingi ili kubaini ukiukwaji wa taratibu uliomfanya mshtakiwa kuendelea kuwekwa ndani bila kupata haki yake ya msingi ya kupewa dhamana.
Hata hivyo, Mawakili wa Jamhuri nao wamewasilisha hoja kindhani juu ya utaratibu uliozingatiwa na kufanya mtuhumiwa kuendelea kuwa ndani bila dhamana.
Kufuatia mawasilisho ya hoja kwa pande zote mbili ambayo yamechua takribani saa nne mbele ya Mh.Jaji Arnold Kirekiano, uamuzi wa ombi hilo umepangwa kutolewa Jumatatu Januari 27, 2025 Saa tatu asubuhi.
Hata hivyo, mshtakiwa Dkt. Slaa amerejeshwa tena rumande huku maombi hayo yakiendelea kusikilizwa.