Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Wakili Peter Madeleka amesema "No Reforms, No Election" haiwezi Kufanywa Uhaini, akisisitiza kuwa madai ya mabadiliko ya kisiasa na kikatiba ni haki ya msingi ya kidemokrasia na sio uchochezi au kosa la jinai. Alifafanua kuwa katika mfumo wa vyama vingi, kila chama kina haki ya kuwa na sera na mtazamo wake kuhusu namna nchi inavyopaswa kuendeshwa na jinsi chaguzi zinavyotakiwa kusimamiwa kwa haki.
Aliongeza kuwa bado kuna changamoto kubwa ya kimfumo ambapo watendaji wengi wa serikali na vyombo vya ulinzi wanaendelea kufanya kazi kwa fikra za kizamani za mfumo wa chama kimoja, wakiamini wajibu wao mkuu ni kukitumikia chama tawala badala ya katiba.
Hali hii inasababisha ubaguzi wa kisiasa ambapo viongozi wa chama tawala wanatoa kauli zenye viashiria vya hatari bila kuchukuliwa hatua, huku upinzani ukikosolewa vikali kwa kudai mageuzi.