Wakili Madeleka: Tuna ushahidi unaojaa fuso mbili polisi kuhusika kumkamata Soka

Wakili Madeleka: Tuna ushahidi unaojaa fuso mbili polisi kuhusika kumkamata Soka

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Maamuzi ya Jaji Wilson Nyansobera yanasubiriwa kutolewa muda sio mrefu kutoka hapa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar Es Salaam juu ya shauri lililoletwa mahakamani na Deusdedith Soka, Jackob Godwin Mlay na Frank Mbise wakiwakilishwa na mawakili Peter Madeleka, Paul Kisabo na Deogratius Mahinyila.

Pia soma: Kutoweka kwa Soka na wenzake, IGP, DPP, OCCID Temeke kufikishwa Mahakamani kwa Hati ya dharura

Jana shauri lilisikilizwa pande zote mbili (upande wa Jamhuri pamoja na waleta maombi) na Jaji Nyansobera alisema maamuzi juu ya shauri hilo atayatoa leo Agosti 28 2024 saa nne asubuhi

Screenshot_2024-08-28-11-56-32-1.png

Mwenyekiti wa Chadema ni miongoni mwa Wananchi Waliohudhuria kesi iliyofunguliwa na Wadau Mbalimbali kuhusu kutekwa kwa Viongozi wa Bavicha Temeke.

Wadau hao wanaomba vijana hao wafikishwe Mahakamani na kushitakiwa ikiwa wanazo tuhuma zozote kwa vile inafahamika kwamba Walikamatwa na Polisi

Hata hivyo Dkt Slaa aliwahi kudokeza njama za Watekaji kupanga kumuua mmoja wa vijana hao na kumtupa kwenye pori moja lililo karibu na DSM, huku Mwenyekiti wa Chadema akimwanika kiongozi wa Watekaji ambaye ni ofisa wa Juu wa Jeshi la Polisi anayeitwa Faustin Mafwele.
 
ivi chadema wamewahi kuishtaki serikali na wakashinda kesi? ukiacha zile ambazo huwa serikali inafungua kuwashtaki lkn wao chadema wakashinda..
 
View attachment 3081302

Mwenyekiti wa Chadema ni miongoni mwa Wananchi Waliohudhuria kesi iliyofunguliwa na Wadau Mbalimbali kuhusu kutekwa kwa Viongozi wa Bavicha Temeke.

Wadau hao wanaomba vijana hao wafikishwe Mahakamani na kushitakiwa ikiwa wanazo tuhuma zozote kwa vile inafahamika kwamba Walikamatwa na Polisi

Hata hivyo Dkt Slaa aliwahi kudokeza njama za Watekaji kupanga kumuua mmoja wa vijana hao na kumtupa kwenye pori moja lililo karibu na DSM, huku Mwenyekiti wa Chadema akimwanika kiongozi wa Watekaji ambaye ni ofisa wa Juu wa Jeshi la Polisi anayeitwa Faustin Mafwele.
View attachment 3081305
Natamani sana kuiona picha ya Faustin Mafwele.
Ni kwa nini Chadema wasimshitaki yeye kama yeye maana wamekwisha mtaja tayari kwenye public kwenye ile press conference ya Mbowe?
 
"Ushahidi unajaa Fuso mbili" unajua maana yake tena ni pamoja na ushahidi wa Kielektroniki.
mkuu cjauliza kuhusu ushahidi mm nimeuliza kama wamewahi kuishtaki serikali na wakashinda kesi..
 
Back
Top Bottom