Wakili Leonard Manyama amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni msingi muhimu wa amani na utulivu wa taifa. Ameyasema hayo Oktoba 10, 2026, katika mdahalo wa Wanasheria kuhusu utawala wa sheria Tanzania.
"Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuliyonayo, kama nilivyosema Ndugu Odemba, ukitaka uone uzuri wa Katiba hii, angalia ni msingi wa amani na utulivu wa taifa letu tuliyonayo. Moja ya kigezo ambacho pia ni kipimo cha kuonyesha kwamba tuna sheria nzuri, tuna katiba nzuri, na tuna utawala unaozingatia haki za binadamu na kanuni zote za utawala bora, ni pamoja na utulivu na amani ya nchi."
Kwa hoja na haiba ya mwonekano wa mzungumzaji nimeamini ccm imeshakuwa dini!
Msomi huwezi kujizima data kiwango hicho!
Usomi ni kujitoa kwenye kifungo cha fikra! Utawaliwe na ukweli!